Kachumbari ya embe na parachichi (mango avocado salsa)

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kusubiri; dakika 30
Muda jumla; dakika 15 na muda wa kusubiri

Mahitaji

Embe 1 kubwa
Parachichi 1 kubwa
Kitunguu maji 1 kidogo
Pilipili kichaa 1
Ndimu 1
Kijiko 1 cha chai tangawizi
Vijiko 2 vya chakula majani ya gilgigilani
Chumvi kwa kuonja

Maelekezo

Katakata embe, parachichi na kitunguu maji vipande vidogovidogo vya mraba; twanga tangawizi; katakata majani ya giligilani na pilipili vipande vyembamba; kamua maji ndimu

Kwenye bakuli ndogo, changanya nusu ya maji ya ndimu na 1/4 kijiko cha chai chumvi. Ongeza kitunguu maji, changanya vizuri; acha ikae kwa dakika kama 10

Kwenye bakuli kubwa, weka embe, tangawizi na pilipili. Ponda kwa kutumia mgongo wa kijiko au potato masher mpaka upate rojo ya embe ila vibakie vipande vipande vya kutafuna

Ongeza parachichi, mchanganyiko wa kitunguu na majani ya giligilani. Ongeza chumvi na maji ya ndimu yaliyobakia kwa kuonja kupata radha utakayoipenda

Funika bakuli, weka kwenye jokofu/ friji; acha ipoe kwa dakika kama 30 au zaidi kabla haijaliwa

Pakua kama utakavyopenda

Enjoy

 

Leave a Reply