Bhajiya za dengu

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kuloweka dengu; masaa 2
Muda wa kupika; dakika 15
Muda jumla; dakika 30 + muda wa kuloweka

Mahitaji

Kikombe 1 dengu
Kitunguu maji 1 kikubwa
Pilipili kichaa 1
¼ kikombe majani ya giligilani/ kotimiri
½ kijiko cha chai red chilli flakes
Kijiko 1 cha chai baking powder
Chumvi kwa kuonja
Mafuta ya kukaangia

Maelekezo

Osha na kuloweka dengu kwa masaa 2

Katakata kitunguu, pilipili na majani ya giligilani

Chuja dengu maji. Weka dengu na maji kiasi (kama vijiko 4-6 vya chakula) kwenye mashine ya kusagia chakula au blender hadi ilainike.  Ikilainika, ongeza kitunguu maji, majani ya giligilani na pilipili kichaa usage kwa sekunde kama 20 hadi 30, visilainike sana

Hamishia mchanganyiko kwenye bakuli kubwa, ongeza baking powder, chumvi nared chilli flakes; changanya vizuri

Chemsha mafuta kwenye kikaango katika moto wa wastani. Chota kijiko kimoja cha chakula kwa kila bhajiya uweke kwenye mafuta yaliyochemka

Kaanga mpaka ziwe crispy na zenye rangi ya kahawia

Toa bajia zilizoiva kwenye mafuta hamishia kwenye sahani iliyowekewa tissues, au chujio la bati ili mafuta yachuje

Pakua za moto au baridi

Enjoy

39 Replies to “Bhajiya za dengu”

  1. Samahani dada Jeni eti pili pili ya kukaushia ndio ipi au ya namna gani wakati u naanza ku blend dengue zako… asante

Leave a Reply