Pancakes za Red Velvet

Mandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 30
Muda jumla; dakika 40

Ingredients

Kikombe 1 unga wa ngano
Vijiko 1-1/2 vya chakula cocoa powder
Kijiko 1 cha chai baking powder
1/4 kijiko cha chai baking soda
1/4 kijiko cha chai chumvi
Kikombe 1 buttermilk
1/4 kikombe sukari 
Yai 1 kubwa
1/2 kijiko cha chai rangi nyekundu ya chakula
Kijiko 1 cha chai vanilla extract
1/4 kikombe siagi, iliyoyeyushwa
Icing sugar ya jibini (Cream Cheese), bonyeza hapa kwa recipe 

Maelekezo

Kwenye bakuli kubwa changanya au chekecha unga wa ngano, cocoa powder, baking soda, baking powder, chumvi na sukari, . Changanya vizuri

Kwenye bakuli jingine, changanya buttermilk, rangi ya chakula, siagi iliyoyeyushwa, yai na vanilla extract mpaka ichanganyike vizuri

Ongeza mchanganyiko kwenye bakuli lenye viungo vikavu. Koroga ichanganyike vizuri

Kwenye kikaangio kisichoshika chini (non-stick), katika moto wa chini, mwagia ¼ kikombe ya unga. Pika mpaka upande wa chini uwe kahawia kwa mbali, na pancake itune kwa juu

Geuza upande wa pili kisha upake siagi upande wa juu ulioiva. Geuza paka siagi na upande wa chini. Pika mpaka iive vizuri. Rudia kwa unga uliobakia mpaka umalize zote

Pakua kama utakavyopenda

Enjoy

One Reply to “Pancakes za Red Velvet”

Leave a Reply