Sausage na mbogamboga za foil

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kupika; dakika 30
Muda jumla; dakika 45

Mahitaji

Sausage na mbogamboga

1/2 kilo sausages
Karoti kubwa 1
Vikombe 2 viazi vidogovidogo
Kitunguu maji 1 kikubwa (vidogo 2)
Uyoga 4 ya wastani
Nusu 3 za hoho (nyekundu, orange na kijani),
Vijiko 4 vya chakula mafuta ya kupikia
1/4 kikombe jibini, ukipenda
Punje 6 kitunguu saumu
Majani ya dania, giligilani au kotimiri ya kuweka juu

Viungo vikavu

1/2 kijiko cha chai basil (mrihani),
1/2 kijiko cha chai rosemary na lavender kavu,
1/2 kijiko cha chai oregano kavu,
1/2 kijiko cha chai kitunguu saumu cha unga
1/2 kijiko cha chai chili pepper flakes
Chumvi kwa kuonja

PS. Unaweza kubadilisha, kuongeza au kupunguza viungo na mbogamboga kutokana na matakwa yako

Maelekezo

Washa oven joto la 200 degrees C. Andaa vipande 3 hadi 4 vya aluminum foil, weka pembeni. Katakata sausage na carroti vipande vya mduara; katakata viazi na uyoga mara nne. Katakata pilipili hoho na kitunguu maji vipande vya mraba; menya kitunguu saumu; weka pembeni

Chemsha viazi kwa dakika kama 3 kisha chuja maji, weka pembeni

Kwenye bakuli kubwa, changanya viungo vyote isipokuwa viazi, changanya hadi vichanganyike vizuri

Ongeza viazi, changanya vizuri

Gawanya mchanganyiko mara tatu, kwenye aluminium foil ulizoandaa. Funga foil vizuri hewa isitoke, ila usiweke kurasa mbili, iwe moja tu

Oka kwa dakika 20

Fungua foil kwa uangalifu, mvuke utatoka ukifungua

Tenga kama utakavyopenda

Enjoy!

8 Replies to “Sausage na mbogamboga za foil”

Leave a Reply