Vipapatio vya kuku vyenye asali na sosi ya soya

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kumarinate; masaa 2
Muda wa kupika; dakika 15
Muda jumla; masaa 2 hours dakika 30

Mahitaji

Kilo 1 vipapatio vya kuku
½ kikombe asali
Kikombe 1 sosi ya soya (low sodium soy sauce)
Vijiko 2 vya chakula mafuta ya kupikia (olive oil)
Vijiko 2 vya chakula siagi
Vijiko 2 vya chakula majani ya giligilani
Kijiko 1 cha chakula kitunguu saumu na tangawizi
Maji ya ½ limao
Chumvi na pilipili manga
Mbegu za ufuta za kunyunyizia kwa juu

Maelekezo

Osha na kukausha kuku. Kata kwenye kiungio cha bawa la kuku upate vipande viwili. Chanja kuku

Katakata majani ya giligilani; kamua maji limao, weka pembeni

Katika bakuli kubwa, changanya vizuri sosi ya soya, tangawizi na kitunguu saumu, majani ya giligilani na maji ya limao. Ongeza vipapatio vya kuku kwenye bakuli, changanya vizuri

Funika bakuli, acha viungo vikolee kwenye jokofu kwa masaa kama 2

Chuja kuku majimaji yote kwenye chujio

Kwenye kikaangio katika moto wa juu kiasi, yeyusha siagi weka na mafuta yachemke pamoja. Ongeza asali, kuku chumvi na pilipili manga kwenye kikaangio

Pika pande zote hadi ziwe na rangi ya kahawia, zinanata na kuiva vizuri; huku ukigeuza mara kwa mara ukipaka mchanganyiko wa sosi kwa juu kila ukigeuza; kama dakika 10

Nyunyizia ufuta kwa juu

Enjoy

4 Replies to “Vipapatio vya kuku vyenye asali na sosi ya soya”

Leave a Reply