Wali wa kukaanga na mayai na minofu ya kuku

Maandalizi; dakika 5
Muda wa kupika; dakika 15
Muda jumla ; dakika 20

Mahitaji

250g/ robo kilo kuku, (aliyepikwa, kuchomwa au kukaangwa)
250g/ robo kilo mchele; uliopikwa
Vijiko 3 vya chakula mafuta
Kijiko 1 cha chai tangawizi na kitunguu saumu
Kitunguu maji 1
Mayai 2
Chumvi kiasi

Maelekezo

Kwenye kikaango katika moto wa wastani, chemsha kijiko 1 cha mafuta. Ongeza kitunguu maji, kitunguu saumu na tangawizi. Kaanga mpaka vilainike

Ongeza kuku, kaanga mpaka kuku akolee viungo vizuri

Hamishia kuku kwenye sahani, weka pembeni

Kwenye kikaango kile kile, ongeza mafuta yaliyobakia. Yakichemka, weka mayai na chumvi. Acha mayai yaive kama utakavyopenda

Ongeza wali na kuku aliyepikwa awali, kaanga mpaka vichanganyikane vizuri

Pakua cha moto

Enjoy

9 Replies to “Wali wa kukaanga na mayai na minofu ya kuku”

Leave a Reply