Chapati za kumimina zenye oatmeal

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 20
Muda kwa jumla; dakika 30

Mahitaji

1/3 kikombe unga wa ngano
1/3 kikombe Oatmeal
Mayai 2
1/4 kijiko cha chai chumvi
Kijiko 1 cha chakula sukari
Kikombe 1 maziwa
Siagi kwa ajili ya kukaangia

Maelekezo

Weka oatmeal kwenye mashine ya kusagia chakula, saga ilainike iwe unga

Kwenye bakuli kubwa changanya unga wa oatmeal, unga wa ngano, mayai, maziwa, chumvi na sukari. Koroga mpaka vichanganyike vizuri

Kwenye kikaango ambacho hakishiki chini katika moto wa wastani, weka robo kikombe unga. Kwa haraka, sambaza vizuri mchanganyiko wako usambae kikaango kizima. Acha ipike hadi kona zikauke zionekane zina rangi ya kahawia kiasi

Kwa kutumia kijiko kipana, geuza chapati upande wa pili, paka siagi upande uliopika

Pika na upande wa chini uive uwe na rangi ya kahawia pia kisha geuza upake siagi. Geuza tena pande zote mpaka iive vizuri. Hamishia chapati kwenye sahani, rudia kwa unga uliobakia

Tenga na chochote utakachopenda wewe

Enjoy

3 Replies to “Chapati za kumimina zenye oatmeal”

Leave a Reply