Korean-Style BBQ Beef

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kumarinate; lisaa 1
Muda wa kupika; dakika 15
Muda jumla; Lisaa 1 dakika 30

Mahitaji

700g steki ya nyama laini
Kitunguu maji 1 kikubwa
Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu
½ pear (peazi)
Vitunguu 3 vya majani
Vijiko 3 vya chakula sukari ya brown
Kijiko 1 cha chai pilipili manga
⅓ kikombe sosi ya soya
Vijiko 3 vya chakula mafuta ya ufuta
Kijiko 1 cha chakula mafuta ya kupikia
Mbegu za ufuta za kunyunyizia
Chumvi ikihitajika

Maelekezo

Katakata nyama vipande vyembamba virefu, weka pembeni kwenye bakuli

Katakata kitunguu maji nusu vipande vyembamba virefu na nusu nyingine vipande vya kawaida; menya na katakata peazi, menya kitunguu saumu, katakata vitunguu vilili vya majani vipande vya mduara na kimoja vipande vya kawaida

Weka nusu ya kitunguu maji ulichokatakata kawaida kwenye blender, ongeza peazi, kitunguu saumu, kitunguu cha majani ulichakatakata vipande vya kawaida, sukari ya brown, pilipili manga, sosi ya soya, na mafuta ya ufuta. Saga mpaka ilainike vizuri. Mwagia mchanganyiko kwenye bakuli la nyama, changanya vizuri

Ongeza kitunguu maji ulichokatakata vipande virefu vyembamba kisha uchanganye vizuri. Funika bakuli, acha viungo vikolee kwa lisaa moja au usiku mzima ndani ya jokofu

Chemsha mafuta kwenye kikaangio katika moto wa juu kiasi. Ongeza mchanganyiko wa nyama

Kaanga mpaka iwe ya kahawia na nyama iive kama utakavyopenda

Pakua, nyunyizia mbegu za ufuta na vitunguu vya majani ulivyokata vipande vya mduara kwa juu. Enjoy na wali au chakula utakachopenda wewe

 

Leave a Reply