Steki na mbogamboga kwenye sosi ya soya na asali

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 20
Muda jumla; dakika 30

Mahitaji

Nyama na mbogamboga

500g/ nusu kilo steki ya nyama (chagua laini)
Vikombe 1½ vya brokoli
Kikombe 1 uyoga
¾ kikombe karoti
Pilipili kichaa nyekundu 1
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja
Vijiko 3 vya chakula mafuta ya mzaituni (olive oil)
½ kikombe kitunguu cha majani
Mbegu za ufuta za kunyunyizia juu

Kwa sosi

¼ kikombe sosi ya soya
½ kikombe maji
¼ kikombe sukari ya brown
Vijiko 2 vya chai kitunguu saumu
Vijiko 2 vya chai tangawizi
Kijiko 1 cha chakula asali
Kijiko cha chai mafuta ya ufuta
Kijiko 1 cha chai na kikoja cha chakula corn flour/ cornstarch

Maelekezo

Hatua ya 1; maandalizi

Katakata nyama vipande virefu vyembamba; katakata brokoli, karoti, pilipili, majani ya kitunguu na uyoga. Twanga kitunguu saumu na tangawiti; weka pembeni

Kwenye bakuli ndogo, changanya corn flour/ cornstarch na vijiko 2 vya chakula maji ya baridi

Hatua ya 2; kutengeneza sosi

Kwenye sufuria ndogo katika moto wa juu kiasi, changanya sosi ya soya, ½ kikombe maji, sukari, tangawizi, kitunguu saumu, asali na mafuta ya ufuta. Pika mpaka sukari iyeyuke kabisa. Ongeza mchanganyiko wa maji na corn flour/ cornstarch. Pika kwa dakika 1 hadi 2 nyingine, au mpaka sosi iwe nzito kabisa. Ipua, weka pembeni

Hatua 3; kupika

Kwenye kikaangio/ sufuria kubwa katika moto mkali kiasi, chemsha mafuta kijiko 1 cha chakula, weka brokoli na karoti. Nyinyizia chumvi na pilipili manga, changanya vizuri. Pika kwa dakika kama 3 ukigeuza mara kwa mara, au mpaka mboga ziive kama utakavyopenda na zianze kupata ukahawia kwa mbali. Hamishia kwenye sahani, weka pembeni

Futa kikaangio, rudisha kwenye moto. Ongeza mafuta vijiko 2 vya chakula, yakichemka weka nyama, nyunyizia chumvi na pilipili manga. (Hakikisha nyama haibebani, kama kikaangia chako ni kidogo pika nusu nusu). Pika pande zote mpaka nyama iive vizuri

Nyama ikiiva, ongeza brokoli, karoti  na uyoga, kwenye kikaangio, changanya vizuri kwa dakika kama 2, kisha weka majani ya kitunguu na pilipili

Ongeza sosi ya soya na iliyopikwa awali. Pika kwa dakika 2 hadi 3 katika moto wa wastani, au mpaka ipate moto vizuri.

Pakua, nyunyizia mbegu za ufuta kwa juu

Enjoy na wali

4 Replies to “Steki na mbogamboga kwenye sosi ya soya na asali”

Leave a Reply