Supu ya Koliflawa

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 30
Muda jumla; Dakika 40

Mahitaji

 1/4 ya koliflawa
Karoti 1 kubwa 
Kijiko 1 cha chakula siagi
Kitunguu 1 kikubwa
Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu na tangawizi
Vijiko 11/2 vya chai vegetable seasoning
Vikombe 2 vya maji ya moto
1/2 kikombe cooking cream
Pilipili manga kwa kuonja 

Maelekezo

Andaa viungo; Katakata koliflawa, kitunguu maji na karoti; menya na kutwanga kitunguu saumu na tangawizi

Kwenye sufuria katika moto wa wastani, yeyusha siagi, ongeza kitunguu saumu na tangawizi; acha viive kwa dakika moja hadi mbili. Ongeza kitunguu maji kiive kwa dakika kama 3, kisiungue

Weka koliflawa na karoti, acha zichanganyikane na viungo vingine kwa dakika chache. Kisha ongeza pilipili manga na vegetable seasoning

 

Punguza moto wa jiko, mimina maji kwenye sufuria. Acha ichemke kwa moto wa chini kwa dakika kama 10-15, au mpaka mboga zilainike vizuri

Toa kwenye moto, acha ipoe kwa dakika 5. Weka mchanganyiko wako kwenye blender au mashine ya kusagia chakula kutengeneza rojo.

Rudisha mchanganyiko kwenye sufuria katika moto wa wastani, ongeza cooking cream, acha iive kwa dakika chache

Pakua na chochote utakachopenda kwa juu

 

Enjoy supu yako!

11 Replies to “Supu ya Koliflawa”

  1. Wow ! Antie jaman nmepika the soup
    Uuwii ni mzuuriii taamuuu saanaa
    I love it to the fullest
    Uishi milele antie Jane😚😘😙

Leave a Reply