Mkate wa ndizi na buttermilk

Maandalizi; dakika 10 
Muda wa kupika; dakika 50 
Muda jumla; lisaa 1

MAHITAJI

1/2 kikombe siagi iliyolainishwa (unsalted butter) 
Kikombe 1 sukari
Mayai 2 makubwa
Kikombe 1 ndizi za kuponda (kama ndizi 2 kubwa)
1/4 kikombe buttermilk
1/2 kijiko cha chai vanilla extract
Vikombe 1 3/4 unga wa ngano
Kijiko 1 cha chai baking powder
1/4 kijiko cha chai chumvi
1/8 kijiko cha chai baking soda

MAELEKEZO

Washa oven joto la 175 C ipate moto. Paka siagi chombo cha kuokea keki, weka pembeni. Ponda ndizi mpaka zilainike vizuri; usitumie mashine tumia mkono, weka pembeni

Kwenye bakuli kubwa, changanya sukari na siagi mpaka ilainike vizuri

Ongeza mayai; moja baada ya jingine huku unachanganya. Koroga mpaka ilainike vizuri

Ongeza buttermilk, ndizi zilizopondwa pamoja na vanilla. Koroga mpaka ichanganyike vizuri

Chekechea unga wa ngano, baking powder, baking soda na chumvi

Koroga vizuri

Mimina mchanganyiko wako kwenye chombo cha kuokea ulichopaka mafuta awali. Oka keki kwa dakika 50; au mpaka iive vizuri

Acha ipoe. Katakata na kutenga kama utakavyopenda

Enjoy

2 Replies to “Mkate wa ndizi na buttermilk”

Leave a Reply