Burger za nyama, cheese na parachichi

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kupika; dakika 15
Muda jumla; dakika 30

Mahitaji

Mahitaji ya nyama

500g/ nusu kilo nyama ya kusaga
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja
Vijiko viwili vya chakula mafuta ya kupikia
Vipande 2-4 vya jibini ya sandwich

Mahitaji ya mkate na viungo vya ndani

Mikate miwili hadi minne ya burger
Siagi ya kukaangia mikate
Kitunguu maji cha wastani
Nyanya moja kubwa
Majani ya salad
Parachichi
Sauce utakazopenda (tomato sauce, mayonnaise au BBQ sauce )

Maelekezo

Katakata kitunguu na nyanya vipande vya mduara; katakata parachichi vipande virefu; osha, katakata na kukausha majani ya salad kwa kutumia kitambaa cha jikoni au tissue za jikoni. (Tafadhali zingatia uoashaji sahihi wa salad kuepuka magonjwa)

Gawanya nyama kwenye madonge mawili (au zaidi kutokana na idadi ya burgers unazotaka). Taratibu yagandamize kwa chini kutengeneza iwe tambarare na ya mduara. Nyunyizia chumvi na pilipili manga kwa juu

Kwenye kikaangio moto mkali kiasi, chemsha mafuta. Weka nyama kwenye kikaangio, upande wenye chumvi na pilipili manga kwa chini kisha nyunyizia  chumvi na pilipili manga kwa upande wa juu pia

Acha nyama iive bila kusumbuliwa wala kugeuzwa kwa dakika 3 hadi 4. Geuza upike na upande mwingine hadi uive kama utakavyopenda. Weka jibini kwa juu sekunde kama 30 kabla ya kutoa nyama kwenye kikaango, au mpaka iyeyuke. Funika kwa sekunde utakazoweka jibini

Kata mkate katikati kisha upake siagi kwa juu kwenye upande wa ndani

Kwenye kikaango katika moto wa wastani, weka mkate upande wenye siagi kwa chini. Kaanga mpaka uwe wa kahawia na ukauke kiasi, angalia usiungue

Ipua mkate, pangilia nyama na viungo vingine kwenye mkate kama utakavyopenda

Enjoy!

18 Replies to “Burger za nyama, cheese na parachichi”

  1. Omg..Jane this is wat i call The VIP BURGER😍 Let me runnnnnn and get some mahitaji🤣🤣🤣 . Before i eat my mobile 😐🤔😨.
    Thank you for saving me Everyday 😙😚

  2. Jins ya kutengeneza hayo maduara ya nyama ya kusaga ndio mtihan….kwan siwez chemsha nyama peke yk???na katika sandwich siwez tumia kabej nikaikata vipande vdgvdg nataka kutengeneza ila haya maduara ndio yamenima mtihan

    1. Maduara tengeneza kwanza donge kama mpira, weka kwenye kibao halafu bonyeza kwa kutumia mkono hadi iwe nyembamba, tumia mkono pia kusawazisha pande zilizopishana. ni rahisi sana ukijaribu. Ukichemsha nyama kabla haitapendeza na haitashikana vizuri. kabeji pia labda uichambue uweke jani zima, ukikatakata haitapendeza tena.

Leave a Reply