Mkate wa Kukaanga na Mayai na Ndizi (Banana French Toast)

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 20
Muda jumla; dakika 30

Mahitaji

Ndizi mbivu 1 kubwa
Mayai 2
Slesi 4 kubwa za mkate
¼ kijiko cha chai tangawizi ya unga
¼ kijiko cha chai mdalasini ya unga
½ kijiko cha chai vanilla extract
Chumvi kiasi
Siagi ya kukaangia

Maelekezo

Ponda ndizi mpaka zilainike vizuri kwa kutumia uma

Ongeza mayai, mdalasini, tangawizi, vanilla na chumvi. Changanya vizuri

Paka siagi kiasi kwenye kikaangio katika moto wa wastani. Loweka mkate kwenye mchanganyiko wa ndizi na mayai hadi ukolee vizuri.

Weka mkate kwenye kwenye kikaango. Pika pande zote mpaka ziwe na rangi ya kahawia ila mkate usikauke wala kuungua

Pakua yamoto. Tenga kama utakavyopenda

Enjoy

3 Replies to “Mkate wa Kukaanga na Mayai na Ndizi (Banana French Toast)”

Leave a Reply