Biskuti za Buttermilk

Matayarisho; dakika 15
Muda wa kupika; dakika 15
Muda jumla; dakika 30

Mahitaji

Vikombe 2 unga wa ngano
Kijiko 1 cha chai chumvi
Kijiko 1 cha chakula baking powder
1/4 kikombe sour cream
1/2 kikombe siagi, iliyogandishwa
3/4 kikombe buttermilk
1 kijiko cha chakula siagi, iliyoyeyushwa

Kutengeneza buttermilk nyumbani 

3/4 kijiko cha chakula siki
3/4 kikombe maziwa

Maelekezo

Washa oven joto la 225 degrees C. Anza kwa kutengeneza buttermilk. Changanya maziwa na siki (vinegar). Koroga vizuri, acha ikae kwa dakika kama 5 kabla hujaitumia

Kwenye bakuli kubwa chekecha unga wa ngano, baking powder na chumvi. Ongeza sour cream, changanya vizuri kwa mikono

Kwangua siagi iliyogandiswa kwenye kifaa cha kukwangulia karoti

Changanya siagi haraka kwenye mchanganyiko wa unga ila isichanganyike sana. Ongeza buttermilk uchanganye, ila usichanganye sana pia. Unga utakuwa unamabonge mabonge kiasi. Hamishia unga kwenye sehemu iliyonyunyiziwa unga. Sukuma kisha katakata kama utakavyopenda kwa kisu au kifaa cha kukatia biskuti

Oka kwa dakika 12 mpaka 14. Toa kwenye oven uzipake siagi iliyoyeyushwa kwa juu. rudisha kwenye oven

Oka kwa dakika 1 nyingine zitakuwa na rangi ya kahawia kwa mbali. Ipua na pakua kama utakavyopenda

Enjoy

4 Replies to “Biskuti za Buttermilk”

Leave a Reply