Pizza ya Tuna Fish na Salami

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 15
Muda jumla; dakika 25

Mahitaji

Mkate 1 wa pizza, jinsi ya kutengeneza bonyeza hapa
Kikombe 1 jibini (Mozzarella cheese)
1/2 kikombe tomato sauce (ukipenda)
1/4 kikombe samaki wa kopo aina ya jodari (Tuna Fish) 
1/4 kitunguu cha wastani
Matunda ya mzaituni meusi (black olives) kiasi
Vipande 4-8 vya Salami 

Maelekezo

Washa oven yako moto wa juu kabisa. Weka unga wa mkate kwenye sehemu iliyonyinyiziwa unga. Acha ukae kwa dakika chache. Jinsi ya kutengeneza unga wa mkate wa pizza bofya hapa 

Sukuma unga wako hadi uwe mwembamba usawa wa chapati nyambamba (itakuwa pana kuliko chapati). Weka kwenye chombo cha kuokea kilichopakwa mafuta au karatasi za kuokea.

Paka tomato sauce kwa juu ya mkate mzima. (unaweza pia kupika bila tomato sauce)

Oka mkate na tomato sauce peke yake kwa dakika kama 8 kisha ongeza viungo vilivyobakia, pangilia kama utakavyopenda

Acha pizza iive kwa dakika 3-4 ; au mpaka jibini iyeyuke na mkate uive kama utakavyopenda. Ipua na kukatakata kama utakavyopenda

Enjoy

4 Replies to “Pizza ya Tuna Fish na Salami”

  1. Thank you chef Jane nakupenda sana na najifunza mengi kutoka kwako.naomba kama unadarasa la whats app niunganishe

Leave a Reply