Unga wa Mkate wa pizza

Muda wa maandalizi; dakika 15
Muda wa kusubiri; masaa 4-5
Muda jumla; dakika 15 + muda wa kusubiri

Mahitaji

Kikombe 1 maji ya uvuguvugu
Vikombe 2-1/3 unga wa ngano
3/4 kijiko cha chai hamira
Vijiko 3 vya chakula mafuta ya kupikia
1/2 kijiko cha chai chumvi
3/4 kijiko cha chai sukari

Maelekezo

Kwenye bakuli la ukubwa wa wastani, weka hamira na maji ya uvuguvugu. Koroga hadi hamira ichanganyike vizuri

Kwenye bakuli kubwa, weka unga wa ngano. Ongeza mchanganyiko wa maji na hamira, pamoja na viungo vingine vyote vilivyobakia

Changanya kila kitu, ukande unga hadi ulainike vizuri. Paka mafuta bakuli jingine pembeni. Weka unga ndani ya bakuli, geuza upande wa juu chini ili pande zote zipate mafuta.

Funika bakuli, acha unga uumuke kwa masaa 4 hadi 5

Kanda unga tena, halafu uugawanye mara mbili. Weka unga kwenye sehemu iliyonyinyiziwa unga. Acha ukae kwa dakika chache kabla ya kutumia

Sukuma iwe mduara mwembamba. Tumia kama itakavyohitajika

Leave a Reply