Keki ya Mdalasini

Maandalizi; dakika 30 
Muda wa kupika; dakika 45 
Muda jumla; saa 1 dakika 15

MAHITAJI

Kwa ajili ya keki

Vikombe 2 unga wa ngano
Kijiko 1 cha chakula baking powder
Kijiko 1 cha chai mdalasini
3/4 kijiko cha chai chumvi
2/3 kikombe siagi
Vikombe 1-1/3 sukari
Vijiko 1-1/2 vya chai vanilla extract
Mayai 3
2/3 kikombe maziwa

Kwa ajili ya sosi ya mdalasini

1/2 kikombe sukari
Vijiko 6 vya chakula siagi
1/3 kikombe maji
Kijiko 1 chai vanilla extract
3/4 kijiko cha chai mdalasini

Maelekezo

Washa oven joto la 175 degrees ipate moto wakati unachanganya keki. Paka siagi chombo cha kuokea keki, weka pembeni. Kwenye bakuli la kubwa, changanya unga wa ngano, mdalasini, chumvi na baking powder weka pembeni

Kwenye bakuli jingine, saga sukari na siagi mpaka ilainike vizuri. Ongeza mayai; moja baada ya jingine huku unachanganya.

Koroga mpaka ilainike vizuri kisha weka vanilla. Changanya vizuri

Ongeza  mchanganyiko wa unga wa ngano kidogo kidogo huku ukichanganya na maziwa. Koroga hadi uchanganyike vizuri

Mimina mchanganyiko wako kwenye chombo cha kuokea ulichopaka mafuta awali. Oka keki kwa dakika 45; au mpaka iive vizuri. Ikiiva, acha ipoe kwa dakika kama 5 kabla ya kuiweka kwenye sahani. Hamishia keki kwenye sahani. Toboa toboa na kijiki wakati bado ya moto kiasi

Weka viungo vyote vya sosi ya mdalasini kwenye sufuria; sukari, maji, siagi, mdalasini na vanilla. Koroga mpaka siagi na sukari viyeyuke vizuri

Mwagia sosi ya mdalasini kwa juu

Katakata na tenga kama utakavyopenda

Enjoy

2 Replies to “Keki ya Mdalasini”

Leave a Reply