Minofu ya kuku na mbogamboga

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kupika; dakika 15
Muda jumla; dakika 30

Mahitaji

Kuku na mbogamboga (unaweza tumia mboga tofauti)

350g minofu ya kuku
Vijiko 2 vya chakula mafuta ya mzaituni
Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu
Kijiko 1 cha chai tangawizi
Karoti 1 kubwa
½ pilipili hoho nyekundu
Kikombe 1 maharagwe machanga
Kikombe 1 uyoga
½ kikombe majani ya kitunguu
¼ kikombe korosho
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja
Mbegu za ufuta kunyunyizia juu

Sosi

Kijiko 1 cha chakula siki (red wine vinegar)
Kijiko 1 cha chakula sosi ya soya
Kijiko 1 cha chakula mafuta ya ufuta
Kijiko 1 cha chakula kitunguu samu na tangawizi
Kijiko 1 cha chakula maji ya ndimu

Maelekezo kwa video

Maelekezo kwa picha

Twanga kitunguu saumu na tangawizi; kamua maji limao

Osha, kausha na katakata nyama vipande virefuvirefu. Changanya nyama na kijiko 1 cha chai tangawizi, kijiko 1 cha chai kitunguu saumu, pilipili manga na chumvi kwa kuonja

Kwenye kibakuli kidogo, changanya viungo vyote vya sosi, weka pembeni

Katakata mbogamboha vipande virefuvirefu; katakata majani ya kitunguu vipande vidogovidogo

Kwenye kikaangio katika moto mkali kiasi, chemsha kijiko 1 cha mafuta ya mzaituni

Ongeza kuku mwenye viungo, kaanga mpaka aive; kama dakika 3-4. (Hakikisha hujazi sana kikaangio, acha kuku aive kwa nafasi. Endapo unatumia kikaangio kidogo, pika nusu nusu)

Kuku akiiva, hamishia kwenye sahani

Rudisha kikaangio kwenye moto, ongeza kijiko 1 cha chakula cha mafuta yaliyobakia katika moto wa juu kiasi. Ongeza karoti na maharagwe machanga, pika kwa dakika 1 hadi 2

Ongeza uyoga na pilipili hoho. Pika kwa dakika moja nyingine (au mpaka ziive kama unavyopenda wewe)

Rudisha kuku kwenye kikaango, changanya vizuri

Mimina mchanganyiko wa sosi

Ongeza korosho na majani ya kitunguu, pika kwa sekunde kama 30

Ipua, nyunyizia mbegu za ufuta. Pakua cha moto

Enjoy

5 Replies to “Minofu ya kuku na mbogamboga”

Leave a Reply