Vipapatio vya kuku vya kukaanga vyenye sosi ya sukari na pilipili

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kupika; dakika 20
Muda jumla; dakika 35

Mahitaji

Kwa kuku

500g / ½ kilo vipapatio vya kuku
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja
½ kijiko cha chai tangawizi ya unga
Vijiko 4 vya chakula potato starch au corn flour
Mafuta ya kukaangia

Kwa sosi

Kijiko 1 cha chakula mafuta
Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu na tangawizi
½ kijiko cha chai chilli pepper flakes (siyo lazima)
Pilipili kichaa 2
Vijiko 2 vya chakula sosi ya soya
Vijiko 4 vya chakula rice syrup au corn syrup
Kijiko 1 cha chai siki nyeupe
Kijiko 1 cha chai mustard (ukipenda)
Kijiko 1 cha chai sukari ya kahawia
Kijiko 1 cha chai mbegu za ufuta
¼ kikombe mbegu za ufuta
Vijiko 2 vya chakula karanga zilizomenywa (siyo lazima)

Maelekezo

Hatua ya 1; andaa kuku na viungo

Katakata majani kitunguu na pilipili; twanga kitunguu saumu

Osha na kukausha vipapatio vya kuku, kisha kata nusunusu, visiwe vizima

Kwenye bakuli kubwa, changanya vipapatio vya kuku, tangawizi ya unga, chumvi na pilipili manga kwa kuonja. Changanya vizuri viungo vishike kwa usawa

Weka potato starch/ corn starch kwenye sahani pana. Paka kuku kipande kimojakimoja mpaka afunikwe kabisa

Hatua ya 2; andaa sosi

Kwenye kikaango kikubwa katika moto wa juu kiasi, chemsha kijiko 1 cha mafuta. Ongeza kitunguu saumu, halafu uweke pilipili kichaa . Pika mpaka vilainike, kama sekunde 30

Ongeza sosi ya soya. Halafu weka rice/corn syrup, chili pepper flakes na mustard. Pika kwa dakika chache ukigeuza mara kwa mara isiungue. Ikichemka vizuri ongeza sukari na siki, pika mpaka sukari iyeyuke. Ipua, weka pembeni

Hatua ya 3; kaanga kuku

Chemsha mafuta kwenye kikaangio katika moto wa juu kiasi. Mafuta yakichemka vizuri, ongeza kuku. Weka kipande kimojakimoja na hakikisha havijazani sana. Kama kikaangio chako ni kidogo, kanga nusunusu. Kaanga mpaka ipate rangi ya kahawia kwa mbali, dakika 8 mpaka 10

Toa kwenye mafuta, weka kwenye chujio au sahani yenye tissues ili mafuta yachuje. Acha ipumzike kwa dakika kama 5

Chemsha tena mafuta, rusisha kuku kwenye mafuta. Kaanga kwa dakika 6 hadi 8 nyingine, au mpaka kuku awe crispy na apate rangi nzuri ya kahawia

Toa kwenye mafuta

Kaanga karanga kwa sekunde 30 mpaka dakika 1, ipua

Hatua ya 4; changanya kuku na sosi

Rudisha sosi kwenye moto, acha ichemke. Ongeza majani ya kitunguu na mbegu za ufuta

Ongeza kuku na karanga. Changanya vizuri

Ipua, enjoy

6 Replies to “Vipapatio vya kuku vya kukaanga vyenye sosi ya sukari na pilipili”

  1. Thank you so much i like your recipes mno nimekuwa nikizijari na familia yangu inafurahia sana. Kwenye acc yako ya instagram nimeweka post notification on ili ukipost tu nione

Leave a Reply