Icing Sugar ya Kupika

Maandalizi; dakika 5
Muda wa kupika; dakika 15
Muda kwa jumla; dakika 20

Mahitaji

Vijiko 5 vya chakula unga wa ngano
Kikombe 1 maziwa
Kikombe 1 sukari nyeupe
Kikombe 1 siagi (butter)
Kijiko 1 cha chai vanilla extract

Maelekezo

Chemsha maziwa na vijiko 5 vya unga wa ngano katika moto wa chini, ukikoroga mfululizo. Acha uchemke mpaka uwe mzito kabisa. Ipua, acha upoe pembeni

Mchanganyiko ukipoa kabisa; Piga sukari na siagi kwenye bakuli kubwa mpaka ilainike vizuri.

Ongeza mchanganyiko wa unga wa ngano na maziwa pamoja na vanilla, endelea kupiga mpaka icing sugar ilainike kabisa

Paka juu ya keki kama itakavyohitajika

Katakata kama utakavyopenda

Enjoy

2 Replies to “Icing Sugar ya Kupika”

Leave a Reply