Chocolate-Chip Cookies

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kusubiri; Usiku kucha
Muda wa kupika; dakika 15
Muda jumla; dakika 30 + muda wa kusubiri

Mahitaji

Vikombe 3 unga wa ngano
Kijiko 1 cha chai baking soda
Kijiko 1 cha chai chumvi
2/3 kikombe siagi iliyoyeyuka kiasi
1/2 kikombe sukari nyeupe
Vikombe 1-1/4 sukari ya brown
Vijiko 2 vya chai vanilla
Mayai 2 makubwa, yasiwe yabaridi
Vikombe 2 chocolate chips

Maelekezo

Kwenye bakuli la kubwa, changanya unga wa ngano, chumvi na baking soda; weka pembeni

Kwenye bakuli jingine kubwa changanya sukari ya brown, sukari nyeupe, siagi, mayai na vanilla mpaka ulainike vizuri. (unaweza kutumia mashine au bila mashine. Ni rahisi zaidi ukitumia mashine)

Changanya mchanganyiko wa unga na mchanganyiko wa sukari. Kanda mpaka uchanganyike vizuri kabisa

Ongeza chocolate chips. Changanya vizuri kisha funika bakuli. Acha unga ulalae kwenye jokofu/ friji usiku kucha uoke kesho yake zitapendeza zaidi. Kama una haraka unaweza kuoka moja kwa moja

Gawanya mchanganyiko wa unga kwa kipimo cha vijiko 3 vya chakula. tengeneza mduara kama vimpira, panga vizuri kwenye chombo cha kuokea ukitumia karatasi za kuokea

Oka kwenye oven iliyopata moto katika joto ya 175 degrees kwa dakika 12-15 au mpaka zianze kupata rangi ya kahawia. Ipua, acha zipoe kabla ya kuhamishia kwenye waya wa kupozea zipoe kabisa

Enjoy

2 Replies to “Chocolate-Chip Cookies”

Leave a Reply