Ice cream rahisi sana ya vanilla

Kutengeneza; dakika 15
Kugandisha; masaa 6
Muda jumla; Masaa 6 dakika 15

Mahitaji

Vikombe 2 whipping cream
Kikombe 1 maziwa ya sona (sweet condensed milk)
Vijiko 2 vya chai vanilla

Maelekezo

Kwenye bakuli kubwa, kwa kutumia mashine ya kusagia keki, piga cream mpaka iwe nzito kabisa

Ongeza maziwa ya sona na vanilla, koroga vizuri kabisa. Unaweza kuendelea na mashine kwa sekunde chache au tumia mkono

Mimina mchanganyiko kwenye contena ya plastic yenye mfuniko au chombo cha kuokea mkate cha bati.

Funika kisha gandisha kwa masaa kadhaa au usiku kucha mpaka igande vizuri kabisa.

Ikiwa tayari kuliwa, acha iyeyuke kwa dakika 5 hadi 10 iwe rahisi kuchota na kijiko

Pakua kama utakavyopenda

Enjoy

Leave a Reply