Kuhusu mimi

Habari, jina langu ni Jane Wambura, mtanzania ninayeishi Berlin nchini Ujerumani. Tangu nipo mtoto mdogo nilipenda sana kupika vyakula tofauti. Mbali na kuwa mpenzi wa chakula kizuri, kupika kunanisaidia pia kutuliza akili. Kwa kupitia blog yangu, ninanata kukuhamasisha ujiunge nami kakika maandalizi ya vyakula tofauti vyenye afya unavyoweza kuandaa mwenyewe nyumbani kwako. Katika blog yangu kutakuwa na mapishi tofauti ya asili ya kiafrika, mapishi ya watu wa wasia, Wamarekani hadi watu wa Ulaya. Ninapenda kukukaribisha kujiunga nami, pamoja tifurahie, tujadili uzoefu wetu pamoja na changamoto za mapishi.

PS: Nitakuwa najibu comments zenu kadri ya uwezo wangu na kuwapa maelezo Zaidi kuliko mapishi yangu kila itakapowezekana