Biryani ni chakula ambacho asili yake kutoka kwa wahindi na waarabu. Ni chakula ambacho mara nyingi huandaliwa siku maalum kama sikukuu, sherehe tofauti, weekends and mikutano ya familia. Chakula hiki kinahitaji muda wa kutosha na umakini katika upikaji ili kuhakikisha kinatoka vizuri na kufurahiwa na walaji. Kumbukumbu yangu ya utoto ni biryani kutengwa kwenye sinia na kuliwa pamoja watoto wengi au familia nzima....yaani gombania goli. Mara nyingi huliwa na kachumbari, vinywaji vya baridi kama soda au juisi pamoja na matunda kama ndizi mbivu na kadhalika. Leo tunatengeza biryani rahisi sana ya kuku ambayo sosi itachanganywa kabisa jikoni na wali
INTROOO

Yaliyomo kwenye ukurasa huu:

Masaa 2 Idadi ya walaji 6 Rahisi

Mambo ya kuzingatia

INTRO
Nyama ya kuku inaweza kutumika ya kuku wa kisasa au wa kienyeji. Ukitumia kuku wa kienyeji hakikisha unaacha aive kwa muda mrefu mpaka nyama ilainike vizuri

Toa ngozi kuku ili viungo vishike vizuri kwenya nyama

Kumarinate kuku ni muhimu sana kwenye pishi hili kwani hufanya nyama ilainike vizuri na kushika viungo vizuri, na pia kuongeza radha vizuri kwenye chakula kizima

Viungo vizimavizima vinafanya biryani inukie na kuwa na radha nzuri zaidi. Unaweza kubadilisha, kuongeza na kupunguza kutokana na upatikanaji wake na upendeleo wa mpishi na walaji

Andaa viungo kabla ya kuanza kupika. Hii itasaidia kutokupika kwa kuharakisha na kuepuka kuunguza chakula. Ukiandaa viungo kabisa ina maana wakati wa kupika utaweka akili yote kwenye kupika, chakula kitatoka vizuri

Moto wa kupikia wakati wa kukaanga nyama na kutengeneza sosi unatakiwa uwe wa wastani ili chakula kisishike chini. Viungo pamoja na maziwa ya mgando husababisha nyama na sosi kushika kwenye sufuria kwa haraka zaidi

Maziwa ya mgando yanasaidia kuongeza ubora na radha ya nyama na pia kufanya sosi uwe na uzito mzuri

Viazi unaweza kuvikaanga kama nilivyofanya au kuacha viive moja kwa moja wakati unapika rosti ya nyama

Vitunguu vya kukaanga unaweza kutumia vya kununua dukani au ukakaanga mwenyewe nyumbani. Kukaanga ni kuweka tu kwenye mafuta mpaka viwe vya kahawia. Unaweza kukaanga vitunguu hata siku kadhaa kabla ya kupika. Unaweza pia kutokuweka vitunguu hivi kama hauvipendi

Kuoka na kupalilia siyo lazima kutumia oven, unaweza pia kuweka kwenye jiko mkaa, uwe mkaa kiasi chini na mwingi zaidi juu.....kama unavyooka keki au mikate
2

Kachumbari na Raita hufanya biryani iwe tamu zaidi. Unaweza kutengeneza kachumbari au raita ya aina yoyote uliyozoea, au angalia recipe zinazofuata

Video

Angalia Video hapa jinsi ya kutengeneza hatua kwa hatua. Usisahau kusubscribe kwenye channel yetu ya YouTube

Mahitaji ya kuku na marinade

Kilo 1 nyama ya kuku
1/2 kikombe maziwa ya mgando
Vijiko 2 vya chakula kitunguu saumu na tangawizi
Vijiko 2 vya chakula maji ya limao
Kijiko 1 cha chai chumvi
Kijiko 1 cha chai paprika
1/2 kijiko cha chai binzari ya manjano
Kijiko 1 cha chakula garam masala

Mahitaji ya wali

Vikombe 3 mchele
Vikombe 6 maji ya kuchemshia mchele
Kijiko 1 cha chai chumvi
Kijiko 1 cha chai mbegu za jira
Star anise 2

Mahitaji ya viungo vya juu

1/3 kikombe maji ya uvuguvugu
1/4 kijiko cha chai saffron strands
1/3 kikombe vitunguu vya kukaanga
Majani ya coriander kama yatakavyohitajika

Mahitaji ya sosi ya kuku

Vijiko 3 mafuta ya kupikia
Vitunguu maji 2 vya wastani
Vijiko 2 vya chakula kitunguu saumu na tangawizi
Kijiko 1 cha chai mbegu za jira
Kipande cha mdalasini
Bay leaves ndogo 4
Karafuu 6
Iliki 6
Nyanya 3 za wastani
Kijiko 1 cha chai garam masala
Kijiko 1 cha chai binzari ya manjano
3/4 kijiko cha chakula coriander powder
1/2 kikombe maziwa ya mgando
Viazi 4 vikubwa
Mafuta ya kukaangia viazi, endapo utavikaanga
Chumvi kama itakavyohitajika

Maelekezo hatua kwa hatua

Hatua ya 1; Marinate kuku

Anza kwa kuosha, toa ngozi, kausha na katakata nyama ya kuku. Ikiwa tayari, chanja chanja kuku ili ukiweka viungo vikolee kila mahali

Endelea kwa kuchanganya viungo vyote vya marinade kwenye bakuli, yani paste kitunguu saumu na tangawizi, maziwa ya mgando, maji ya limao, paprika, binzari ya manjano, garam masala pamoja na chumvi. Changanya vizuri

Weka nyama ya kuku kwenye baluli la viungo, changanya vizuri nyama ishike na kukolea viungo vizuri. Funika, weka kwenye friji kwa lisaa 1 au usiku mzima. Inapendeza zaidi ikikaa usiku mzima

Hatua ya 2; Andaa Mchele

Ukiwa tayari kupika, osha mchele mara kadhaa mpaka maji yawe masafi. Loweka kwenye maji masafi kwa muda wa kama nusu saa. Yaani acha mchele uloane wakati unaanza kupika wali

Hatua ya 3; Vingo vya juu

Changanya maji na saffron strands, acha vilowane wakati unapika nyama

Kama utaumia vitunguu maji vya kukaanga mwenyewe, ndiyo muda wa kukaanga sasa, ili viwe tayari. Unaweza pia kukaanga kabla vikae tu tayari

Katakata majani ya koriander, weka pembeni

Hatua ya 4; Pika kuku

Anza hatua hii kwa kuandaa viungo kabisa. Menya na katakata viazi, katakata vitunguu maji vipande virefu nyembamba na pia saga nyanya au katakata vipande vidogo vidogo sana, upendeleo wako

Muda wa kupika kuku ukifika, anza kwa kuweka mafuta kwenye kikaango katika moto wa juu kiasi ili yachemke. Yakichemka ongeza kitunguu maji, kitunguu saumu na tangawizi, iliki, karafuu, mdalasini na mbegu za jira

Kaanga mpaka vitunguu maji vianze kupata rangi ya kahawia na harufu ya ubichi iishe kwenye paste ya kitunguu saumu na tangawizi

C0007T01

Ongeza nyama ya kuku uliyomarinate. Iweke kwa kusambaza kwenye kikaango, isibebane. Kaanga kwa dakika kama 4 au mpaka ipate rangi ya kahawia kwa mbali, geuza upande wa pili ukaange kwa dakika kama 2-3 nyingine. Kumbuka hapa nyama haitakiwi kuiva, ni kuibadilisha tu rangi kidogo kwa juu. Itaiva na nyanya

Ukishageuza nyama upande wa pili, ongeza nyanya zilizoandaliwa pamoja na viungo vya unga ambavyo ni garam masala, coriander powder, binzari ya manjano pamoja na chumvi. Changanya vizuri kisha funika acha nyama iive imefunikwa mpaka nyanya ziive vizuri. Kumbuka viungo na maziwa ya mgando husababisha nyama kushika chini kwa haraka, hivyo ni vizuri kuigeuza nyama mara kwa mara kuhakikisha haishiki chini

Nyanya zikiiva, ongeza maziwa ya mgando. Changanya vizuri kisha funika tena kikaango, acha nyama iive moto wa wastani au wa chini mpaka sosi ianze kukaukia, ibakie kiasi sana ya kuwivishia wali ukiweka kwenye oven

C0010T01

Hatua ya 5; Kaanga viazi

Kaanga viazi kwenye mafuta mpaka viive vizuri viwe na rangi nzuri ya kahawia

Ongeza viazi kwenye mchanganyiko wa sosi ya nyama, changanya vizuri

Hatua ya 6; Chemsha mchele

Wakati nyama inaiva na unakaanga viazi, weka mchele pamoja na mbegu za jira, star anise na chumvi kwenye maji yanayochemka. Acha uchemke mpaka ukaribie kuiva, ila usiive kabisa

Ipua mchele, chuja maji kisha weka pembeni tayari kwa kuoka/ kupalilia

Hatua ya 7; Oka/ palilia biryani

Washa oven moto wa 150 degrees C ipate moto kwa dakika kama 15 kabla ya kuweka biryani

Weka rosti ya nyama uliyochanganya na viazi kwenye chombo cha kuokea, isambaze vizuri chini. Ongeza wali kwa juu huku ukiusambaza kuhakikisha nyama yote imefunikwa. Nyunyizia maji ya saffron kwa juu kisha sambaza vitunguu vya kukaanga na majani ya coriander kwa juu kabisa

Funika na aluminium foil au kama ni chombo chenye mfuniko, funika vizuri ikaze kabisa. Oka kwa dakika kama 20-30, au mpaka wali uive kabisa

Ukiiva toa kwenye oven, changanya vizuri. Biryani yako itakuwa tayari

02

Hatua ya 8; Enjoy

Pakua kama utakavyopenda

Comments

Join discussion.