Biskuti rahisi sana za kuyeyuka zenyewe mdomoni zinazotengenezwa kwa viungo vitano tu. Ukijaribu mara moja hutazichoka tena

Yaliyomo kwenye ukurasa huu:

Dakika 30 Idadi ya walaji 6 Rahisi

Mambo ya kuzingatia

Vipimo ni muhimu sana katika kuoka. Kama unataka matokeo mazuri katika uokaji, fuatilia vipimo kama vilivyo, kamwe usikadirie chochote. Tumia vikombe na vijiko maalum kwa kupimia ili kupata matokea mazuri zaidi

Siagi ni muhimu sana kwa hizi biskuti, ndio maana zinaitwa za siagi. Siagi zinapatikana supermarkets karibu zote. Jaribu kununua siagi ya bila chumvi (unsalted)

Icing sugar ni muhimu sana kwenye uokaji hizi biskuti kwa sababu inasaidia zisisambae sana katika uokaji, zitoke na umbo zuri pia.

Vanilla siyo muhimu sana kwenye hii recipe ingawa inaongeza radha nzuri. Endapo hutaipata hauna haja ya kuogopa kuoka bila vanilla

Unga wa ngano upimwe bila kuzidisha. Kikombe kipimwe na juu kusiwe na mlima, kuwe na usawa. Unga ukizidi biskuti zitatoka kavu na zitamong´onyoka

Kwenye kuoka, ili kupata biskuti nzuri hakikisha umewasha oven na imepata joto kabla ya kuoka. Pia hakikisha oven imewasha kwenye setting ya joto la juu na chini

Ukitoa kwenye oven biskuti zitakuwa laini sana, ziache zikae kwa dakika kama tano kwenye chombo cha kuokea, kisha hamishia kwenye waya wa kupozea mpaka zipoe kabisa

Hifadhi biskuti kwenye air tight container kwa wiki moja sehemu ya kawaida au mpaka miezi 3 ndani ya freezer

Video

Angalia Video hapa jinsi ya kutengeneza hatua kwa hatua. Usisahau kusubscribe kwenye channel yetu ya YouTube

Mahitaji

Kikombe 1 siagi
1/2 kikombe icing sugar
Kijiko 1 cha chai vanilla extract
Vikombe 2 unga wa ngano
1/4 kijiko cha chai chumvi

Maelekezo hatua kwa hatua

Hatua ya 1

Anza kwa kuwasha oven joto la 175 degrees C ili ipate joto wakati unachanganya unga. Kwenye bakuli kubwa changanya siagi, icing sugar na chumvi mpaka mchanganyiko ulainike vizuri. (unaweza kutumia mashine au bila mashine. Ni rahisi zaidi ukitumia mashine).

Hatua ya 2

Ongeza vanilla, changanya kwa dakika kama moja nyingine

Hatua ya 3

Ongeza unga wa ngano. Kanda mpaka uchanganyike vizuri kabisa

Hatua ya 4

Gawanya mchanganyiko wa unga kwa kipimo cha kijiko 1 cha chakula, tengeneza mduara kama vimpira. Panga vizuri kwenye chombo cha kuokea ukitumia karatasi za kuokea. Hakikisha umeacha nafasi ya kutosha katikati ya kila biskuti. Kandamiza kila donge la biskuti kwa kutumia cookies stamp, uma, glasi ya maji au kifaa chochote utakachotumia kutengeneza umbo unalotaka

Hatua ya 5

Hakikisha unachovya kifaa cha kutengenezea umbo la biskuti kwenye icing sugar ili kusaidia unga usinate kwenye kifaa na pia umbo litokee vizuri zaidi

Hatua ya 6

Oka kwenye oven iliyopata moto katika joto ya 175 degrees kwa dakika 12-15 au mpaka zianze kupata rangi ya kahawia chini. Usishangae zikiwa laini sana wakati unazitoa kwenye oven, ni kawaida zikipoa zinakuwa kawaida

Hatua ya 7

Ipua, acha zipoe kwa dakika 5 kabla ya kuhamishia kwenye waya wa kupozea zipoe kabisa

Comments

Join discussion.