Chapati ni chakula pendwa kinachoweza kuliwa wakati wowote; kama kitafunwa cha chai asubuhi na vilevile kama chakula kikuu cha mchana au usiku ambacho unaweza kusindikiza na mboga tofauti au supu
Yaliyomo kwenye ukurasa huu:
Lisaa 1 | Idadi ya chapati 6 | Rahisi |
Mambo ya kuzingatia
Vipimo Jaribu kufuatilia vipimo kama vilivyo. Tumia vikombe na vijiko maalum kwa kupimia ili kupata matokea mazuri zaidi
Unga wa ngano unaweza kuhitajika zaidi kidogo kutokana na ukandaji wa unga. Kama utakanda na mashine unaweza ukawa mlaini sana. Ikitokea umekuwa mlaini sana, ongeza kijiko kimojakimoja mpaka uache kunata
Icing sugar inasaidia kuleta radha nzuri na rangi nzuri wakati wa kukaanga. Haifanyi chapati ziwe tamu sana kwa hiyo usiogope kutumia. Unaweza pia kutumia sukari ya kawaida badala ya icing sugar
Corn starch/ corn four inasaidia kwenye kulainisha chapati. Zinapatikana kwa urahisi sana madukani. Endapo utakosa kabisa, usiweke, badala yake ongeza unga kama 1/4 kikombe ili usiwe mlaini sana
Siagi inaongeza radha na kulainisha chapati. Chapati zinapendeza sana pia na mafuta ya samli endapo utakuwa nayo. Unaweza pia kutumia mafuta ya kawaida au blue band badala ya siagi
Kusukuma na kukata kama inavyoonyesha kwenye video inasaidia chapati zichambuke vizuri. Unaweza pia kukata na kukunja kwa njia nyingine tofauti
Muda wa kusubiri kwenye kila hatua unasaidia kurahisisha kukanda unga, kusukuma na kufanya chapati ziwe laini zaidi. Ukiwa hauna muda, unaweza kukanda unga moja kwa moja, na kusubiri kwa dakika 10-20 baada ya kukunja kabla ya kukaanga
Funika chapati na plastic wrap au kitambaa, weka kwenye hot pot au oven yenye joto la chini ili ziendelee kuwa za moto na pia zilainike wakato bado unachoma nyingine. Mwanzoni zinaweza kuwa crispy kiasi, zinavyoendelea kukaa zinalainika
Hifadhi chapati kwenye friji. Ukitaka kula tena, pasha kwenye microwave kwa sekunde kama 40 mpaka dakika 1 au pasha kwenye kikaanga cha moto kwa dakika kama 1 au mpaka zipate joto. Baada ya kupasha zitalainika tena!
Video
Angalia Video hapa jinsi ya kutengeneza hatua kwa hatua. Usisahau kusubscribe kwenye channel yetu ya YouTube
Mahitaji
Vikombe 3-1/2 unga wa ngano; na wa ziada wa kusukumia
1/2 Kijiko cha chai chumvi
1/3 kikombe corn flour
Vijiko 2 vya chakula icing sugar
Vijiko 3 vya chakula siagi; na ya ziada ya kukunjia na kukaangia
1/2 kikombe maziwa ya mtindi
Kikombe 1 maji ya kawaida
Maelekezo hatua kwa hatua
Hatua ya 1
Weka unga wa ngano, chumvi, icing sugar na corn flour kwenya bakuli kubwa. Changanya vizuri
Hatua ya 2
Ongeza vijiko 3 vya siagi iliyoyeyushwa. Tumia mikono kuchanganya, uwe kama unasugua kwenye viganja vya mikono mpaka ichanganyikane vizuri
Hatua ya 3
Ongeza maziwa ya mgando/ mtindi pamoja na maji. Kanda mpaka uchanganyikane tu. Kisha funika bakuli, acha unga utulie kwa dakika kama 10-20
Hatua ya 4
Dakika 10-20 zikipita. Kanda tena unga mpaka ulainike vizuri kabisa. Ugawanye kwenye madonge kama 6 yaliyolingana. Unaweza pia kufanya kubwa zaidi au ndogo zaidi. Funika tena, acha utulie kwa dakika 10-20. Kuuacha unasaidia kurahisisha kwenye kusukuma na pia kulainisha chapati zaidi
Hatua ya 5
Dakika 10-20 zikipita, sukuma unga mpaka uwe mpana ukubwa zaidi ya chapati. Paka siagi kwa juu kisha nyunyizia unga wa ngano kiasi. Katakata vipande vyembamba kadri utakavyoweza, kisha vikusanye uikunje kama unavyokunja chapati. Funika tena kwa dakika kama 20 ili unga ulainike uwe rahisi kusukuma
Hatua ya 6
Sukuma unga kwa kutumia mikono, usitumie kijiti cha kusukumia chapati. Ukisukuma na mkono zinachambuka zaidi. Usiogope, kusukuma kwa mkono ni rahisi sana kama inavyoonekana kwenye video
Hatua ya 7
Kaanga pande zote, paka na siagi kila utakapogeuza kila upande
Hatua ya 7
Pakua, funika na kitambaa cha jikoni. Unaweza pia kuweka kwenye hotpot, oven yenye joto au kufunika na plastic wrap



Comments
Join discussion.