Kwa wapenzi wa chocolates chip cookies, unahitaji recipe moja tu kwenye maisha yako. Jaribu hii hutojutia

Yaliyomo kwenye ukurasa huu:

Dakika 40 Idadi ya cookies 20-26 Rahisi

Mambo ya kuzingatia

Vipimo ni muhimu sana katika kuoka. Kama unataka matokeo mazuri katika uokaji, fuatilia vipimo kama vilivyo, kamwe usikadirie chochote. Tumia vikombe na vijiko maalum kwa kupimia ili kupata matokea mazuri zaidi

Siagi ni muhimu ikiwa imelainika kabla ya kutumia. Itoe kwenye friji lisaa moja kabla ya kuanza kuchanganya na viungo vingine. Siagi pia zinapatikana supermarkets karibu zote. Jaribu kununua siagi ya bila chumvi (unsalted)

Unga wa ngano upimwe bila kuzidisha. Kikombe kipimwe na juu kusiwe na mlima, kuwe na usawa

Kwenye kuoka, ili kupata biskuti nzuri hakikisha umewasha oven na imepata joto kabla ya kuoka. Pia hakikisha oven imewasha kwenye setting ya joto la juu na chini

Ukitoa kwenye oven cookies zitakuwa laini sana, ziache zikae kwa dakika kama tano kwenye chombo cha kuokea, kisha hamishia kwenye waya wa kupozea mpaka zipoe kabisa

Hifadhi cookies kwenye air tight container kwa siku hadi 5 sehemu ya kawaida au mpaka miezi 3 ndani ya freezer

Video

Angalia Video hapa jinsi ya kutengeneza hatua kwa hatua. Usisahau kusubscribe kwenye channel yetu ya YouTube

Mahitaji

Vikombe 3 unga wa ngano
Kijiko 1 cha chai baking soda
Kijiko 1 cha chai chumvi
Kikombe 1 siagi iliyolainika
1/2 kikombe sukari nyeupe
Vikombe 1-1/4 sukari ya brown
Kijiko 1 cha chakula vanilla
Mayai 2 makubwa, yasiwe yabaridi
Vikombe 2 chocolate chips

Maelekezo hatua kwa hatua

Hatua ya 1

Kwenye bakuli kubwa, changanya unga wa ngano, chumvi na baking soda; weka pembeni

Hatua ya 2

Kwenye bakuli jingine kubwa weka sukari ya brown, sukari nyeupe na siagi. Changanya mpaka ilainike vizuri kabisa. Ongeza mayai na vanilla, endelea kuchanganya mpaka mchanganyiko ulainike vizuri

Hatua ya 3

Ongeza mchanganyiko wa unga kidogokidogo kwenye bakuli la mchanganyiko wa siagi, sukari na mayai. Endelea kuchanganya mpaka uchanganyike vizuri kabisa

Hatua ya 4

Ongeza chocolate chips kwenye mchanganyiko wa unga. Changanya vizuri kisha funika bakuli na karatasi ya kufunikia chakula. Weka unga kwenye friji/ jokofu kwa muda wa masaa 24 mpaka 72

Hatua ya 5

Ukiwa tayari kuoka, washa oven joto la 170 degrees C moto wa juu na chini. Acha oven ipate moto wakati unaandaa cookies

Hatua ya 6

Gawanya mchanganyiko wa unga kwa kipimo cha vijiko 3 vya chakula. tengeneza mduara kama vimpira, panga vizuri kwenye chombo cha kuokea ukitumia karatasi za kuokea

Hatua ya 7

Oka kwenye oven iliyopata moto katika joto ya 17o degrees C kwa dakika 12-15 au mpaka zianze kupata rangi ya kahawia chini. Usishangae zikiwa laini sana wakati unazitoa kwenye oven, ni kawaida zikipoa zinakuwa kawaida

Hatua ya 8

Ipua, acha zipoe kwa dakika 5 kabla ya kuhamishia kwenye waya wa kupozea zipoe kabisa

Comments

Join discussion.