Hizi ni cookies unazoweza kuzikata kwa maumbo tofauti na kuzipamba kwa icing sugar tofauti na mapambo mbalimbali. Kwa wenye familia haswa watoto, zinafaa sana kutengeneza pamoja katika vipindi vya sikukuu tofauti

Yaliyomo kwenye ukurasa huu:

Kuandaa masaa 5; Kuoka dakika 12 Idadi ya cookies 20-26 Rahisi

Mambo ya kuzingatia

Vipimo ni muhimu sana katika kuoka. Kama unataka matokeo mazuri katika uokaji, fuatilia vipimo kama vilivyo, kamwe usikadirie chochote. Tumia vikombe na vijiko maalum kwa kupimia ili kupata matokea mazuri zaidi

Siagi ni muhimu ikiwa imelainika kabla ya kutumia. Itoe kwenye friji lisaa moja kabla ya kuanza kuchanganya na viungo vingine. Siagi pia zinapatikana supermarkets karibu zote. Jaribu kununua siagi ya bila chumvi (unsalted)

Unga wa ngano upimwe bila kuzidisha. Kikombe kipimwe na juu kusiwe na mlima, kuwe na usawa

Kwenye kuoka, ili kupata cookies nzuri hakikisha umewasha oven na imepata joto kabla ya kuoka. Pia hakikisha oven imewasha kwenye setting ya joto la juu na chini

Oka muda mfupi kulingana na maelekezo. Ukizidisha muda cookies zinakauka zinakuwa hazipendezi tena

Ukitoa kwenye oven cookies zitakuwa laini sana, ziache zikae kwa dakika kama tano kwenye chombo cha kuokea, kisha hamishia kwenye waya wa kupozea mpaka zipoe kabisa

Hifadhi mchanganyiko wa unga kwenye friji kwa lisaa moja mpaka siku 2. Mimi ninapenda kuweka masaa 24, kama una haraka lisaa 1-2 yanatosha

Hifadhi cookies kwenye air tight container kwa siku hadi 5 sehemu ya kawaida, siku 10 kweye friji au mpaka miezi 3 ndani ya freezer

Video

Angalia Video hapa jinsi ya kutengeneza hatua kwa hatua. Usisahau kusubscribe kwenye channel yetu ya YouTube

Mahitaji

Vikombe 2-1/4 unga wa ngano
1/2 Kijiko  cha chai baking powder
1/4 kijiko  cha chai chumvi
3/4 kikombe siagi iliyolainika
3/4 kikombe sukari nyeupe
Yai 1
1/2 kijiko cha chai vanilla
1/4-1/2 kijiko cha chai almond extract (siyo lazima)

Maelekezo hatua kwa hatua

Hatua ya 1

Kwenye bakuli kubwa, changanya unga wa ngano, chumvi na baking powder; weka pembeni

Hatua ya 2

Kwenye bakuli jingine kubwa weka sukari na siagi. Changanya mpaka ilainike vizuri kabisa. Ongeza yai, endelea kuchanganya mpaka mchanganyiko ulainike vizuri. Wakati wa kuchanganya kumbuka kukwangua mchanganyiko utakaoruka pembeni kwenye bakuli, ili kila kitu kichanganyikane vizuri

Hatua ya 3

Ongeza vanilla na almond extract, changanya tena vizuri kwa dakika kama 1 nyingine

Hatua ya 4

Ongeza mchanganyiko wa unga. Endelea kuchanganya mpaka uchanganyike vizuri kabisa. Kuepuka kuchafua jiko, kama unatumia mashine kuchanganya, changanya kwanza na mwiko au kijiko baada ya kuweka unga ili unga usisambae jikoni

Hatua ya 5

Gawanga mchangayiko wa unga kwenye madonge 2. Sukuma katikati ya vipande viwili vya nailoni za jikoni (plastic wraps), angalia video kwa maelekezo vizuri zaidi. Hamishia kwenye sahani kisha weka unga kwenye friji/ jokofu kwa muda wa lisaa 1 au masaa 2; au mpaka siku 2. Mimi binafsi napenda kuandaa usiku nioke siku inayofuata zinapendeza zaidi

Hatua ya 6

Ukiwa tayari kuoka, washa oven joto la 175 degrees C moto wa juu na chini. Acha oven ipate moto wakati unaandaa cookies

Hatua ya 7

Katakata cookies na vifaa vya kukatia utakavyopenda. Unga utakao bakia, uchanganye tena na mkono, sukuma huku unanyunyizia unga wa ngano, endelea kukata mpaka unga wote uishe. Weka kuku kwenye chombo cha kuokea chenye karatasi za kuokea (baking papers) kama unazo, ukikosa, weka kwenye chombo kilichopakwa mafuta na kunyunyizia unga kwa juu

Hatua ya 8

Oka kwenye oven iliyopata moto katika joto ya 175 degrees C kwa dakika 12 au mpaka zianze kupata rangi ya kahawia chini. Usishangae zikiwa laini sana wakati unazitoa kwenye oven, ni kawaida zikipoa zinakuwa kawaida

Hatua ya 9

Ipua, acha zipoe kwenye chombo cha kuokea kwa dakika 5 kabla ya kuhamishia kwenye waya wa kupozea zipoe kabisa

Hatua ya 10

Acha cookies zipoe. Zikiwa tayari, unaweza kula kama zilivyo au kuzipamba na icing sugar utakayopenda

Comments

Join discussion.