Hizi ni cookies zinazohitaji viungo vichache vya kawaida lakini zina ulaini wa kuyeyuka zenyewe mdomoni na radha nzuri sana ya nazi. Ukijaribu hutoacha kuzioka tenaDSC08732

Yaliyomo kwenye ukurasa huu:

Kuandaa dakika 20; Kuoka dakika 20 Idadi ya cookies 12 Rahisi sana

Mambo ya kuzingatia

Vipimo ni muhimu sana katika kuoka. Kama unataka matokeo mazuri katika uokaji, fuatilia vipimo kama vilivyo, kamwe usikadirie chochote. Tumia vikombe na vijiko maalum kwa kupimia ili kupata matokea mazuri zaidi

Siagi ni muhimu ikiwa imeyeyuka kabla ya kutumia. Iyeyushe kwenye microwave au bakuli juu ya maji ya moto. Hakikisha haipati moto, inayeyuka tu. Siagi pia zinapatikana supermarkets karibu zote.

Sukari unaweza kuongeza ikawa 1/2 kikombe kama unapenda ziwe tamu zaidi au punguza mpaka 1/4 kikombe endapo hupendi sukari kabisa.

Unga wa mahindi upo maalum kwa kuokea. Ukiukosa tumia wa kawaida.

Machicha ya nazi tumia ya kununua supermarkets au madukani ambayo yameshakaushwa, au ukiweza kausha mwenyewe nyumbani. Tumia yasiyo na sukari, endapo utapata ya sukari unaweza kupunguza kipimo cha sukari kiasi kama hupendi ziwe tamu sana

Unga wa mahindi na corn flour vipimwe bila kuzidisha. Kikombe kipimwe na juu kusiwe na mlima, kuwe na usawa

Kwenye kuoka, ili kupata cookies nzuri hakikisha umewasha oven na imepata joto kabla ya kuoka. Pia hakikisha oven imewasha kwenye setting ya joto la juu na chini
DSC08713
Oka kwa dakika 20 kulingana na maelekezo. Ukizidisha muda cookies zitakauka na zinakuwa hazipendezi tena

Ukitoa kwenye oven cookies zitakuwa laini sana, ziache zikae kwa dakika kama tano kwenye chombo cha kuokea, kisha hamishia kwenye waya wa kupozea mpaka zipoe kabisa

Hifadhi cookies kwenye air tight container kwa siku hadi 5 sehemu ya kawaida, siku 10 kweye friji au mpaka miezi 3 ndani ya freezer

Video

Angalia Video hapa jinsi ya kutengeneza hatua kwa hatua. Usisahau kusubscribe kwenye channel yetu ya YouTube

Mahitaji

Kikombe 1 unga wa mahindi
Kikombe 1 corn flour
1/2 kikombe machicha ya nazi
1/3 kikombe sukari
1/2 kikombe siagi iliyoyeyushwa
Yai 1

Maelekezo hatua kwa hatua

DSC08737

Hatua ya 1

Kwenye bakuli kubwa, changanya unga wa mahindi, corn flour, machicha ya nazi na sukari. Changanya mpaka uchanganyikane vizuri kabisa

Hatua ya 2

Weka kashimo katikati ya mchanganyiko wa unga, ongeza siagi iliyoyeyushwa na yai lililopigwa

Hatua ya 3

Kanda vizuri mpaka unga uwe donge zuri laini, halitakuwa laini sana

Hatua ya 4

Gawanya kwenye madonge 12 yaliyolingana. Unaweza kupima kwa kutumia kijiko cha chakula 1-1/2 hadi 2

Hatua ya 5

Viringisha kila donge liwe mduara vizuri, kisha bonyeza katikati juu na chini kuwe kama usawa wa kawaida. Angalia video kwa kuelewa zaidi

Hatua ya 6

Pamba au kubonyeza na uma, glass au kifaa chochote utakachopendezwa nacho

Hatua ya 7

Weka kwenye chombo cha kuokea chenye baking paper. Kama huna baking paper, paka chombo mafuta kisha nyinyizia unga wa mahindi kiasi kwa juu

Hatua ya 8

Oka kwenye oven iliyopata moto katika joto ya 170 degrees C kwa dakika 20 au mpaka zianze kupata rangi ya kahawia chini. Usishangae zikiwa laini sana wakati unazitoa kwenye oven, ni kawaida zikipoa zinakuwa kawaida

Hatua ya 9

Ipua, acha zipoe kwenye chombo cha kuokea kwa dakika 5 kabla ya kuhamishia kwenye waya wa kupozea zipoe kabisa

Hatua ya 10

Enjoy na kinywaji cha moto au baridiiii

Comments

Join discussion.