Fruit salad huandaliwa mara nyingi katika siku maalum kama weekends na familia, siku za sikukuu, siku za shughuli muhimu na kadhalika. Fruit salad hunoga zaidi baada ya kufurahia chakula kizuri, unashushia kama dessert. Mara nyingi fruit salad inaongezewa na viungo vingine tofauti kama soda, yogurt, custard, condensed milk na kadhalika ili kuongeza radha. Leo tutaweka matunda peke yake na kiungo cha siri cha kuboresha radha kitakuwa ni asaliDSC09463

Yaliyomo kwenye ukurasa huu:

Dakika 20 Idadi ya walaji 2 Rahisi

Mambo ya kuzingatia

Aina ya matunda inategemea na mtengenezaji, walaji pamoja na msimu. Tumia matunda yanayopatikana na unayoyapenda wewe

Matunda sahihi ni yale ambayo hayajaiva sana. Yawe yameiva tu vizuri lakini siyo ya kubondeka ukichanganya. Matunda mazima mazima yanapendeza zaidi kuliko yaliyorojeka

Usafi ni muhimu sana kwenye utengenezaji wa fruit salad kwani ni rahisi sana kupata magonjwa kwenye utengenezaji wa matunda. Tumia cutting board kwenye ukataji kuepuka kushikashika matunda, pia osha na kukausha matunda vizuri kabla ya kukatakata

Hifadhi kwenye friji wakati unasubiri wakati wa kula

Asali siyo nzuri kiafya kwa watoto wa chini wa mwaka mmoja. Zingatia afya ya watoto kama una watoto wadogoDSC09472

Video

Angalia Video hapa jinsi ya kutengeneza hatua kwa hatua. Usisahau kusubscribe kwenye channel yetu ya YouTube

Mahitaji

C0282T01
Chungwa 1
Strawberries 6
3/4 kikombe zabibu mchanganyiko
Kikombe 1 papai
1/2 ndizi kubwa
1/2 apple
Kiwi 1
Embe 1 dogo

Maelekezo hatua kwa hatua

Hatua ya 1

Kamua maji ya machungwa, weka pembeni

Hatua ya 2

Osha na kukatakata matunda vipande vinavyokaribia kulingana. Vipande havitalingana vyote kwa sababu matunda yapo tofauti

Hatua ya 3

Weka matunda yaliyokatwakatwa kwenye bakuli kubwa. Ongeza asali na maji ya machungwa. Changanya vizuri

Hatua ya 4

Funika bakuli, weka kwenye friji mpaka wakati wa kula.
C0283T01-1

Comments

Join discussion.