Ginger-garlic paste ni kati ya viungo muhimu sana kwenye mapishi, na pia inaongeza radha kwa asilimia kubwa kwenye vyakula tofauti. Paste hii pia inasaidia katika mmeng´enyo wa chakula na pia kulainisha nyama katika mapishi mbalimbali. Ingawa zinapatikana kwa wingi madukani, ni rahisi sana pia kutengeneza majumbani. Jaribu recipe yetu utupe mrejesho

Yaliyomo kwenye ukurasa huu:

Dakika 15 Rahisi

Mambo ya kuzingatia

Tangawizi zipo za aina mbili; zenye ukali sana na zisizo kali sana. Ukitumia zile kali sana hakikisha unaweka vitunguu saumu vingi zaidi yani badala ya 1/4 kilo weka 1/2 kilo. Ukichanganya na tangawizi kali kwa usawa na kitunguu saumu utaharibu radha na pia itakuwa chungu

Mafuta ni muhimu kwenye kutengeneza paste. Mafuta yanasaidia ikae muda mrefu bila kuharibika. Unaweza pia kuweka chumvi au binzari ya manjano ukipenda badala ya mafuta

Maji yanasaidia kurahisisha kwenye kusaga kutokana na mashine unayotumia. Kama mashine yako ina nguvu sana, huna haja ya kuweka maji

Hifadhi kwenye chupa safi yenye mfuniko kwa mwezi mmoja ndani ya friji; au weka kwenye vikopo vya ice cubes uweke kwenye freezer kwa mpaka miezi 6. Ukihitaji unatoa cube moja au zaidi kutokana na uhitaji wako

Video

Angalia Video hapa jinsi ya kutengeneza hatua kwa hatua. Usisahau kusubscribe kwenye channel yetu ya YouTube

Mahitaji

1/4 kilo kitunguu saumu
1/4 kilo tangawizi
1/8 kikombe mafuta ya kupikia
Maji kiasi sana

Maelekezo hatua kwa hatua

Hatua ya 1

Osha na kukatakata tangawizi. weka pembeni

Hatua ya 2

Menya vitunguu saumu

Hatua ya 3

Weka viungo vyote kwenye mashine ya kusagia, saga mpaka ilainike vizuri kabisa. Endapo mashine yako ni ndogo, saga kidogokidogo mpaka umalize

Hatua ya 4

Hifadhi kwenye chupa inayofunga vizuri au kwenye vikopo vya ice cubes uweke kwenye freezer kwa muda mrefu zaidi

Comments

Join discussion