Ukitaka kuwa mtaalam wa kutengeneza ice cream, unahitaji tu kujua kutengeneza ice cream ya vanilla, na kuongeza utundu wako mwenyewe kwa kutumua viungo na upambaji tofauti

Yaliyomo kwenye ukurasa huu:

Masaa 6 Dakika 15 Idadi ya walaji 6 Rahisi

Mambo ya kuzingatia

Matumizi ya cream. ukitaka ice cream iwe nzuri na laini tumia whipped cream zinapatikana madukani. Ukitumia maziwa ice cream inakuwa kama barafu

Ugandishaji. Ukitaka ice cream yako igande vizuri bila mabonge au vipande vya barafu, hakikisha imefunikwa vizuri kwenye air tight container au ukitumia chombo cha mkate cha bati, hakikisha kimefunikwa vizuri na plastic wrap (nailoni za kufunikia chakula) ambayo unaweza kununua supermarkets na madukani

Radha tofauti Kwa kufuata recipe ya ice cream ya vanilla, unaweza kutengeneza ice cream nyingine nyingi tofauti. Ongeza cookies kama oreo uziponde uchanganye, au ndizi mbivu, embe la kusaga, strawberries na vitu vingine tofauti kupata radha tofauti

Video

Angalia Video hapa jinsi ya kutengeneza hatua kwa hatua. Usisahau kusubscribe kwenye channel yetu ya YouTube

Mahitaji

Vikombe 2 whipping cream
Kikombe 1 maziwa ya sona (sweet condensed milk)
Vijiko 2 vya chai vanilla

Maelekezo hatua kwa hatua

Hatua ya 1

Kwenye bakuli kubwa, kwa kutumia mashine ya kusagia keki, piga cream mpaka iwe nzito kabisa

Hatua ya 2

Ongeza maziwa ya sona na vanilla, koroga vizuri kabisa. Unaweza kuendelea na mashine kwa sekunde chache au tumia mkono

Hatua ya 3

Mimina mchanganyiko kwenye contena ya plastic yenye mfuniko au chombo cha kuokea mkate cha bati

Hatua ya 4

Funika kisha gandisha kwa masaa kadhaa au usiku kucha mpaka igande vizuri kabisa.

Hatua ya 5

Ikiwa tayari kuliwa, acha iyeyuke kwa dakika 5 hadi 10 iwe rahisi kuchota na kijiko

Hatua ya 6

Pakua kama utakavyopenda kwa kuipamba na matunda, chocolates, syrups na kadhalika

Comments

Join discussion.