Mango-Avocado-Salsa ni kachumbari ya matunda; yani embe na parachichi ikaongezewa na kitunguu maji, pilipili isiyowasha (unaweza kuweka ya kuwasha pia), tangawizi pamoja na maji ya ndimu. Mbali na utamu uliopitiliza, kachumbari hii pia ni nzuri sana kiafya kwani inatengenezwa na viungo fresh vyenye virutubisho mwilini. Kachumbari hii inaweza kuliwa na kila kitu wakati wowote. Unaweza kula kama kifungua kinywa pamoja na sausages, mikate, mayai n.k, au na chakula kikuu kama pilau, wali, biryani, nyama choma, samaki choma na kadhalika!
ok1-1

Yaliyomo kwenye ukurasa huu:

Dakika 30 Idadi ya walaji 2 Rahisi

Mambo ya kuzingatia

ok
Embe ni vizuri liwe limeiva lina juisi ya kutosha kuweka mchuzimchuzi, ila lisiwe limerojeka sana kuharibu muonekano mzima wa kachumbari

Parachichi linafaa liwe limeiva vizuri na halijarojeka, liwe na vipande vizima vizima visivyopondeka ukichanganya na embe

Kitunguu maji kinapendeza zaidi kikioshwa na kuondolewa ukali. Unaweza kuosha kawaida kwa kusugua na chumvi au osha na siki (vinegar)

Maji ya ndimu yanapendeza zaidi kuliko maji ya limao. Endapo utakosa ndimu tumia limao bado itakuwa nzuri

Majani ya koriander yanaboresha muonekano na kuongeza radha kwenye kachumbari. Weka kiasi utakachopenda wewe

Tangawizi pia inaboresha radha ya kachumbari. Kuwa muangalifu usiweke nyingi sana ikaharibu radha na kuweka ukali kama wa pilipili

Pilipili kichaa siyo ya kuwasha, inaongeza na kuboresha radha ya kachumbari. Unaweza kuongeza pilipili ya kuwasha kiasi ukipenda

Viungo vya ziada kama pilipili manga na kadhalika vinaweza kuongezwa kuboresha radha na muonekano

Usafi ni muhimu sana kwenye utengenezaji wa vyakula vya matunda kwani ni rahisi sana kupata magonjwa kwenye utengenezaji wa matunda. Tumia cutting board kwenye ukataji kuepuka kushikashika matunda, pia osha na kukausha matunda vizuri kabla ya kukatakata

Video

Angalia Video hapa jinsi ya kutengeneza hatua kwa hatua. Usisahau kusubscribe kwenye channel yetu ya YouTube

Mahitaji

2018200005
Embe 1 kubwa
Parachichi 1
Kitunguu maji 1 kidogo
Pilipili kichaa 1
Ndimu 1
Kijiko 1 cha chai tangawizi
Vijiko 2 vya chakula majani ya Koriander
Chumvi kwa kuonja

Maelekezo hatua kwa hatua

Hatua ya 1

Anza kwa kuosha na chumvi au kuloweka kitunguu maji kwenye vinegar wakati unaandaa viungo vingine

Hatua ya 2

Osha, kausha na katakata embe, parachichi na kitunguu maji vipande vidogovidogo vya mraba; twanga tangawizi; katakata majani ya giligilani na pilipili vipande vyembamba; kamua maji ndimu.
2018500005

Hatua ya 3

Kwenye bakuli kubwa, weka embe, tangawizi na pilipili. Ponda kwa kutumia mgongo wa kijiko au potato masher mpaka upate rojo ya embe ila vibakie vipande vipande vya kutafuna

Hatua ya 4

Ongeza parachichi, mchanganyiko wa kitunguu na majani ya giligilani. Ongeza chumvi na maji ya ndimu kidogokidogo kwa kuonja kupata radha utakayoipenda

Hatua ya 5

Funika bakuli, weka kwenye jokofu/ friji; acha ipoe kwa dakika kama 30 au zaidi kabla haijaliwa

Hatua ya 6

Pakua kama utakavyopenda na enjoy
20182900005

Comments

Join discussion.