Kuku mrahisi anayevutia na kupendezesha meza pia; mahsusi kwa siku maalum au kwa chakula cha kila siku
Yaliyomo kwenye ukurasa huu:
Masaa 4 | Idadi ya walaji 4 | Rahisi |
Mambo ya kuzingatia
Washa oven dakika kama 10 mpaka 15 uhakikishe imepata moto kabisa kabla ya kuweka kuku. Unaweza pia kumchoma kuku kwenye grill au jiko la mkaa
Osha kuku na kumkausha na tissues za jikoni kabla ya kumpaka viungo na kumuoka
Siagi ni muhimu sana kwenye uokaji wa huyu kuku kwani anaongeza kwenye kufanya alainike vizuri na pia kuongeza radha ya kuku
Viungo vinaweza kuongezwa kutokana na matakwa ya mpishi na walaji
Weka kuku waya wa chini katika oven, usiweke katikati. Kuku ni mkubwa ukiweka katikati atapata moto zaidi juu kusababisha asiive vizuri
Kausha ngozi ya kuku kwa kuongeza moto kwenye oven dakika za mwisho kama utapenda awe wa brown zaidi na ngozi ikauke zaidi
Video
Angalia Video hapa jinsi ya kutengeneza hatua kwa hatua. Usisahau kusubscribe kwenye channel yetu ya YouTube
Mahitaji
Kuku 1 mkubwa
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja
1/4 kikombe siagi iliyolainika
Vijiko 3 vya chakula olive oil
Vijiko 2 vya chakula paste tangawizi na kitunguu saumu
1/2 kijiko cha chai paprika
1/2 limao
Maelekezo hatua kwa hatua
Hatua ya 1
Osha na kukausha kuku kwa kutumia tissues za jikoni kisha umpake chumvi kwa juu ya ngozi. Tenganisha ngozi na minofu ya kuku upake chumvi na ndani ya kuku ili minofu ikolee chumvi vizuri pia. Angalia video kwa maelekezo zaidi
Hatua ya 2
Changanya siagi iliyolainika, mafuta (olive oil), paste ya kitunguu saumu na tangawizi, paprika na maji ya limao. Changanya vizuri
Hatua ya 3
Paka vizuri mchanganyiko viungo kwenye kuku. Anza kwa kumpaka ndani, katikati ya ngozi kisha umpake kwa juu mpaka kuku mzima apate viungo
Hatua ya 4
Nyunyizia pilipili manga kwa juu ya kuku kiasi utakachopenda
Hatua ya 5
Funika kuku, acha akae kwenye friji kwa masaa kama mawili au kama una muda wa kutosha, acha akae usiku kucha
Hatua ya 6
Ukiwa tayari kuoka, washa oven joto la 200 degrees C kwa dakika kama 10 ili oven ipate moto kwabla ya kuweka kuku. Oka kwa lisaa kama moja, fungua oven, rudishia mafuta yatakayomwagikia kwenye chombo cha kuokea juu ya kuku. Mpake kote ili asitoke mkavu. Rudisha kwenye oven kwa kama nusu saa nyingine
Hatua ya 7
Ipua, acha apoe kwa dakika kama 5 kabla ya kuliwa. Enjoy



Majadiliano
embedd discussion component here.
Comments
Join discussion.