Sidhani kama ninafahamu mtu hata mmoja asiyependa kuku. Kuku anapendwa na watu wengi na pia ana mapishi mengi sana. Karibuni tujaribu wa kukaanga na viungo vikavu kwa leo, hamtojutia kujaribu recipe hii
Yaliyomo kwenye ukurasa huu:
Dakika 40 | Idadi ya walaji 4 | Rahisi |
Mambo ya kuzingatia
Katakata kuku katika vipande 8, yani kila kiungo kionekane vizuri. Hii unaongeza ubora na mvuto kwatika mapishi. Angalia video kuona jinsi nilivyomkata kuku
Kukoleza viungo kwa kuacha kwenye friji usiku mzima kama una muda kunaongeza radha nzuri zaidi kwenye kuku. Kuku anayewekewa tangawizi na kitunguu saumu hulainika vizuri pia, kwa hiyo ukikaanga atakuwa crispy (kaukau) nje na mlaini ndani; ndiyo lengo letu kubwa
Viungo vinavyokosekana mahali ulipo mbali na unga wa ngano, kitunguu saumu na tangawizi vinaweza kubadilishwa. Unaweza pia kuongeza viungo vingine mbalimbali ambavyo unavipenda na umevizoea
Moto wakati wa kukaanga usiwe mkali sana ukababua kuku nje akatoka mbichi ndani. Moto ukiwa mdogo sana pia kuku atanyonya mafuta na hatakauka vizuri. Hakikisha moto ni sahihi katika kukaanga
Usijaze sana kikaango acha kuku waive kwa nafasi na usawa. Kama una kikaango kidogo, pika kidogokidogo ila kuhakikisha wanaiva vizuri
Hakikisha mafuta yamechemka vizuri wakati unaweka kuku. Mafuta yasipochemka vizuri kuku atanyonya mafuta wakati wa kula utakinai na hutafurahia. Mafuta yasiyocheka pia yanafanya kuku asikauke vizuri
Tissues za jikoni au gazeti ni muhimu sana unapotoa kuku kwenye mafuta. Huu husaidia kufyonza mafuta yaliyobakia ili kuku asiwe na mafutamafuta wakati wa kula
Video
Angalia Video hapa jinsi ya kutengeneza hatua kwa hatua. Usisahau kusubscribe kwenye channel yetu ya YouTube
Mahitaji
Kuku 1 mkubwa
Vijiko 2 vya chakula paste tangawizi na kitunguu saumu
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja
Vijiko 6 vya chakula unga wa ngano
Vijiko 1½ vya chai tangawizi ya unga
Vijiko 2 vya chakula chicken bouillon powder
Mafuta ya kukaangia
Maelekezo hatua kwa hatua
Hatua ya 1
Osha, katakata na kuchanja kuku kisha umpake paste ya kutunguu saumu na tangawizi. Tumia mikono kuhakikisha viungo vimeshika kipande kizima. Ongeza chumvi na pilipili manga, rudia tena kupaka vizuri kwenye kila kipande uhakikishe viungo vimeshika vizuri. Kama muda unaruhusu, funika kuku weka kwenye friji kwa masaa kadhaa au usiku kucha kabla ya kukaanga ili viungo vikolee vizuri na kuku alainike
Hatua ya 2
Chemsha mafuta kwenye kikaangio moto wa juu kiasi. Wakati mafuta yanachemka, malizia kuandaa kuku. Kwenye sahani pana, weka unga wa ngano, chicken flavor/ bouillon powder na tangawizi ya unga, changanya vizuri
Hatua ya 3
Paka vizuri mchanganyiko wa unga kwa juu na hakikisha kuku amefunikwa kila mahali
Hatua ya 4
Mafuta yakichemka, weka kuku kwenye mafuta, hakikisha hujazi sana kikaangio, acha waive kwa nafasi. Endapo kikaangio ni kidogo, pika kidogokidogo
Hatua ya 5
Acha kuku aive bila kugeuzwa kwa dakika kama 2 hadi 3 au hadi awe na rangi ya kahawia kiasi na mkavu kwa juu. Unaweza kuongeza na kupunguza moto ikibidi. Geuza kuku upande wa pili, acha aive kwa dakika nyingine 2 hadi 3; au mpaka uhakikishe kuku ameiva vizuri kabisa. Geuza kila inapobidi
Hatua ya 6
Kuku akiiva, hamishia kwenye wire rack, chujio la bati au karatasi za jikoni ili mafuta yachuje kabla hajaliwa.
Hatua ya 7
Enjoy na chakula utakachopenda



Majadiliano
embedd discussion component here.
Comments
Join discussion.