Maharagwe ni mboga pendwa yenye virutubisho vingi sana inayoliwa karibu kila siku kwa karibu kila familia. Mbali na kupendwa sana, kuna wakati unaweza kuyachoka. Kuepuka kuyachoka, unaweza kubadilisha jinsi unavyoyapika na viungo unavyotumia

Yaliyomo kwenye ukurasa huu:

Dakika 30 Idadi ya walaji 4-6 Rahisi

Mambo ya kuzingatia

Maharagwe yachemshwe yaive kabisa kabla ya kuunga kwani kwenye kuunga unatumia muda mfupi sana. Unaweza pia kutumua maharagwe ya aina tofauti kwa recipe hii

Nyanya fresh zinapendeza zikiwa kiasi sana. Usiweke nyingi zikaharibu radha ya maharagwe. Kuna wengine hawapendi nyanya kwenye maharagwe. Unaweza pia usitumie, tumia ya kopo peke yake badala yake au usiweke kabisa. Kwangua au saga nyanya ili kupata rosti nzuri zaidi

Nyanya ya kopo inasaidia kuongeza uzito na radha kwenye maharagwe. Usiweke nyingi sana ikaharibu radha. Unaweza pia kutokuitumia ukikosa

Vegetable flavor unaweza kutokutumia endapo hutaipata. Weka chumvi badala yake. Kumbuka vegetable flavor ina chumvi pia, kama utatumia unaweza usihitaji chumvi kabisa

Tui la nazi nimetumia la kununua siyo ya kukuna nyumbani. Ukiweka tui kwenye maharagwe punguza moto ili isishike chini na kuuguza maharagwe

Maji siyo lazima kuweka. Endapo utaridhika na uzito wa tui la nazi unaweza kutokuweka maji

Video

Angalia Video hapa jinsi ya kutengeneza hatua kwa hatua. Usisahau kusubscribe kwenye channel yetu ya YouTube

Mahitaji

1/2 kilo maharagwe yaliyochemshwa
Vijiko 2 vya chakula mafuta ya kupikia
Kitunguu maji 1 kikubwa
Nyanya 1 kubwa
Kijiko 1 cha chakula vegetable flavor
Kijiko 1 cha chai binzari ya manjano
Kijiko 1-1/2 cha chakula nyanya ya kopo
Chumvi kwa kuonja
1/2 kikombe tui la nazi
1/2 maji

Maelekezo hatua kwa hatua

Hatua ya 1

Anza kwa kuandaa viungo. Katakata kitunguu maji vipande vidogovidogo vya mraba. Kwangua au saga nyanya, weka pembeni

Hatua ya 2

Ukiwa tayari kupika, chemsha mafuta kwenye sufuria. Ongeza kitunguu maji, kaanga mpaka kilainike ila kisikauke wala kuungua. Kiive tu

Hatua ya 3

Ongeza nyanya, nyanya ya kopo, vegetable flavor na binzari ya manjano. Changanya vizuri, funika sufuria kwa dakika kama 5 au mpaka nyanya ziive vizuri. Funua sufuria, geuza nyanya

Hatua ya 4

Ongeza maharagwe, tui la nazi na maji. changanya vizuri kisha funika tena. Punguza moto yaive moto wa chini kwa dakika kama 3 mpaka 5, au mpaka sosi ichemke vizuri na iwe na uzito utakaopenda. Unaweza usiweke maji kama utaoenda iwe nzito sana

Hatua ya 5

Ongeza chumvi endapo itahitajika. Kumbuka vegetable flavor ina chumvi tayari

Hatua ya 6

Pakua ya moto na chakula utakachopenda

Comments

Join discussion.