Kuku ni ndege anayependwa sana na anakuja na mapishi mengi ya aina tofauti. Minofu ya mapaja ya kuku (chicken thighs) ni nyama laini sana na inapendeza kwenye mapishi tofauti. Leo tutaikaanga na paste ya kitunguu saumu na tangawizi pamoja na paprika ya unga. Nyama hii ni tamu na laini sana, na pia inafaa kuliwa na chakula cha aina yoyote!DSC00081-1

Yaliyomo kwenye ukurasa huu:

Dakika 40 Idadi ya walaji 2 Rahisi

Mambo ya kuzingatia

Kuku wa kienyeji anafaa pia kwa recipe hii. Kwenye kukaanga itabidi ukaange poto wa chini kwa muda mrefu zaidi. Kumbuka kuku wa kienyeji hatokuwa mlaini sana kama wa kisasa

Kitunguu saumu na tangawizi ni kiungo muhimu sana kwenye hili pishi. Unaweza kuongeza au kupunguza kutokana na matakwa ya mpishi na walaji

Sufuria au kikaangio cha non-stick kinafaa zaidi kwenye hili pishi kwani kitunguu saumu husababisha nyama kunata chini kwenye sufuria ya kawaida

Muda wa kumarinate ni kuanzia nusu saa mpaka masaa 48. Usiache nyama ikae kwenye friji kwa zaidi ya masaa 48, itaharibika. Na nyama inapendeza zaidi ikikaa usiku kucha kwenye friji. Unaweza pia kutengeneza na kuweka kwenye freezer mpaka utakapokuwa tayari kutumiaDSC00124-1

Viungo tofauti mbali na paprika vinaweza kuongezwa kutokana na matakwa ya mpishi na walaji. Unaweza kuongeza pilipili, limao na kadhalika

Nyama tofauti na minofu ya kuku inaweza kutumika kwenye hili pishi. Unaweza kutumia kifua cha kuku, nyama ya ngĀ“ombe, mbuzi, kondoo, kitimoto au samaki. Vile vile unaweza kuchoma nyama badala ya kuikaanga

Moto wa wastani unafaa zaidi kwenye ukaangaji wa huyu kuku. Moto mkali sana utafanya nyama ibabuke na isiive vizuri ndani. Moto wa chini sana pia utafanya nyama idode isitoke vizuri

Video

Angalia Video hapa jinsi ya kutengeneza hatua kwa hatua. Usisahau kusubscribe kwenye channel yetu ya YouTube

Mahitaji

1/2kg minofu ya mapaja ya kuku (baada ya kutoa ngozi na mifupa)
Vijiko 3-4 vya chakula olive oil
Vijiko 2 vya chakula paste ya kitunguu saumu na tangawizi
Kijiko 1 cha chai paprika ya unga
Chumvi kama itakavyohitajika
Pilipili manga kama itakavyohitajika

Maelekezo hatua kwa hatua

Hatua ya 1

Anza kwa kuandaa viungo. Changanya vijiko 2-3 vya chakula olive oil, kitunguu saumu na tangawizi, paprika, na pilipili manga kwenye bakuli

Hatua ya 2

Unaweza kununua nyama ya bila ngozi na mifupa, ikitokea umepata ya kawaida, toa ngozi na mifupa mwenyewe kisha uchanje chanje minofu kama kwenye video hapo juu

Hatua ya 3

Changanya nyama na viungo uliyotengeneza awali. Ongeza na chumvi kisha uchanganye tena. Unaweza kuweka chumvi kabla, mimi ninaweka badae ili kuhakikisha haizidi wala kupungua baada ya kuona wingi wa nyama

Hatua ya 4

Funika kuku, weka kwenye friji kwa nusu saa au mpaka usiku kucha. Jinsi anavyokaa muda mrefu ndiyo jinsi anavyozidi kupendeza.

Hatua ya 5

Weka kuku kwenye kikaangio chenye kijiko 1 cha mafuta yaliyochemka katika moto wa wastani. Acha aive upande mmoja hadi awe na rangi ya kahawia, asiungue; geuza upande wa pili, acha apike hadi aive vizuri, angalia asikauke

Hatua ya 6

Pakua ya moto na chakula utakachopenda; au acha ipoe kabisa kama utatumia kwenye saladDSC00084-1

Comments

Join discussion.