Kama una ndizi zimeiva zinaelekea kuoza huna haja ya kuzitupa, hizo ndio siri ya radha nzuri na utamu katika mkate wa ndizi

Yaliyomo kwenye ukurasa huu:

Saa 1 Idadi ya walaji 8 Rahisi

Mambo ya kuzingatia

Vipimo ni muhimu sana katika kuoka. Kama unataka matokeo mazuri katika uokaji, fuatilia vipimo kama vilivyo, kamwe usikadirie chochote. Tumia vikombe na vijiko maalum kwa kupimia ili kupata matokea mazuri zaidi

Buttermilk inaweza kuwa changamoto kupata lakini zinapatikana supermarkets. Endapo utakosa unaweza kutengeneza mwenyewe nyumbani kwa kuchanganya kikombe 1 cha maziwa fresh na kijiko 1 cha chakula cha siki nyeupe (white vinegar). Acha ikae kwa dakika 5 kisha tumia kama kawaida

Ndizi ni kiungo muhimu sana katika uokaji wa mkate wa ndizi. Ndizi zilizoiva sana hata kama unahisi zinakaribia kuharibika ila hazijaoza ndio zinapendezesha mkate wa ndizi zaidi. Kama unanunua ndizi fresh, chagua zilizoiva kupitiliza

Mayai na Siagi kama unahifadhi kwenye friji, hakikisha umetoa lisaa moja kabla ya kutumia. Siagi ikilainika inachanganyikana vizuri zaidi na mayai pamoja na viungo vingine na vilevile kuongeza keki kuchambuka vizuri zaidi. Mayai pia yanachanganyikana vizuri yakiwa siyo ya baridi. Mayai ya baridi yanasababisha viungo vingine kama siagi kuganda na kufanya keki isichambuke vizuri. Endapo umejisahau kutoa kwenye friji, lainisha siagi kwe kuweka kwenye kibakuli juu ya maji ya moto kwa dakika moja au mbili. Kwa mayai, toa kwenye friji kisha weka kwenye maji ya uvuguvugu (siyo ya moto) kwa dakika

Baking powder na baking soda zina matumizi tofauti katika uokaji. Katika recipe hii unahitaji zote, baking powder na baking soda

Kuoka hakikisha umewasha oven moto wa juu na chini na oven imepata joto kabla ya kuweka kwenye oven. Hakikisha pia oven hujawasha moto mkali sana ili keki iive vizuri ndani na isiungue nje

Hifadhi keki kwenye kontena kwa siku hadi tatu nje ya friji au siku 6 kwenye friji

Video

Angalia Video hapa jinsi ya kutengeneza hatua kwa hatua. Usisahau kusubscribe kwenye channel yetu ya YouTube

Mahitaji

1/2 kikombe siagi iliyolainishwa (unsalted butter)
Kikombe 1 sukari
Mayai 2 makubwa
Kikombe 1 ndizi za kuponda (kama ndizi 2 kubwa)
1/4 kikombe buttermilk
1/2 kijiko cha chai vanilla extract
Vikombe 1 3/4 unga wa ngano
Kijiko 1 cha chai baking powder
1/4 kijiko cha chai chumvi
1/8 kijiko cha chai baking soda

Maelekezo hatua kwa hatua

Hatua ya 1

Washa oven joto la 175 C ipate moto. Paka siagi chombo cha kuokea keki, weka pembeni. Ponda ndizi mpaka zilainike vizuri; usitumie mashine tumia mkono, weka pembeni

Hatua ya 2

Chekechea unga wa ngano, baking powder, baking soda na chumvi

Hatua ya 3

Kwenye bakuli kubwa, changanya sukari na siagi mpaka ilainike vizuri

Hatua ya 4

Ongeza mayai; moja baada ya jingine huku unachanganya. Koroga mpaka ilainike vizuri

Hatua ya 5

Ongeza buttermilk, ndizi zilizopondwa pamoja na vanilla. Koroga mpaka ichanganyike vizuri

Hatua ya 6

Ongeza mchanganyiko wa unga wa ngano kwenye bakuli, koroga hadi uchanganyike vizuri. Angalia usikoroge sana na kwa muda mrefu. koroga mpaka mchanganyiko uchanganyike vizuri tu

Hatua ya 7

Mimina mchanganyiko wako kwenye chombo cha kuokea ulichopaka mafuta awali. Oka kwa dakika 55; au mpaka mkate uive vizuri. Ukiiva, acha upoe kwenye chombo cha kuokea kwa dakika chache kisha hamishia kwenye waya wa kupozea keki upoe kabisa

Comments

Join discussion.