Ndizi ni moja ya matunda yanayopatikana kwa wingi na pia zinaiva haraka sana na kuharibika kiurahisi. Kuoka mkate wa ndizi ni njia mojawapo wa kutumia ndizi haswa zile zinazokaribia kuharibika.

Yaliyomo kwenye ukurasa huu:

Saa 1 Idadi ya walaji 8 Rahisi

Mambo ya kuzingatia

Vipimo ni muhimu sana katika kuoka. Kama unataka matokeo mazuri katika uokaji, fuatilia vipimo kama vilivyo, kamwe usikadirie chochote. Tumia vikombe na vijiko maalum kwa kupimia ili kupata matokea mazuri zaidi

Ndizi ni kiungo muhimu sana katika hii keki. Ndizi zilizoiva sana hata kama unahisi zinakaribia kuharibika ila hazijaoza ndio zinapendezesha mkate wa ndizi zaidi. Kama unanunua ndizi fresh, chagua zilizoiva kupitiliza

Mayai na Siagi kama unahifadhi kwenye friji, hakikisha umetoa lisaa moja kabla ya kutumia. Siagi ikilainika inachanganyikana vizuri zaidi na mayai pamoja na viungo vingine na vilevile kuongeza keki kuchambuka vizuri zaidi. Mayai pia yanachanganyikana vizuri yakiwa siyo ya baridi. Mayai ya baridi yanasababisha viungo vingine kama siagi kuganda na kufanya keki isichambuke vizuri. Endapo umejisahau kutoa kwenye friji, lainisha siagi kwe kuweka kwenye kibakuli juu ya maji ya moto kwa dakika moja au mbili. Kwa mayai, toa kwenye friji kisha weka kwenye maji ya uvuguvugu (siyo ya moto) kwa dakika

Baking powder na baking soda zina matumizi tofauti katika uokaji. Katika recipe hii unahitaji baking soda siyo baking powder

Chocolate chips zinapatikana supermarkets au kwenye maduka ya vitu vya kuokea keki. Unaweza pia kutumia matunda kama zabibu kavu, berries na kathalika badala ya chocolate chips

Kuoka hakikisha umewasha oven moto wa juu na chini na oven imepata joto kabla ya kuweka kwenye oven. Hakikisha pia oven hujawasha moto mkali sana ili keki iive vizuri ndani na isiungue nje

Hifadhi keki kwenye kontena kwa siku hadi tatu nje ya friji au siku 6 kwenye friji

Video

Angalia Video hapa jinsi ya kutengeneza hatua kwa hatua. Usisahau kusubscribe kwenye channel yetu ya YouTube

Mahitaji

Ndizi 3 zilizoiva sana
1/3 kikombe siagi iliyoyeyushwa
1/2 kikombe sukari
Yai 1 lililopigwa
Kijiko 1 cha chai vanilla extract
Kijiko 1 cha chai tangawizi
Kijiko 1 cha chai baking soda
1/4 kijiko cha chai chumvi
Vikombe 1 ½ unga wa ngano
½ kikombe chocolate chips

Maelekezo hatua kwa hatua

Hatua ya 1

Washa oven joto la 180 C ipate moto. Paka siagi chombo cha kuokea keki, weka pembeni. Ponda ndizi mpaka zilainike vizuri; usitumie mashine tumia mkono

Hatua ya 2

Ongeza siagi, sukari, yai, vanilla, tangawizi, baking soda na chumvi. Koroga mpaka ichanganyikane vizuri kabisa

Hatua ya 3

Ongeza unga wa ngano, changanya mpaka uchanganyikane vizuri

Hatua ya 4

Ongeza chocolate chips. Changanya vizuri

Hatua ya 5

Mimina mchanganyiko wako kwenye chombo cha kuokea ulichopaka mafuta awali. Oka kwa dakika 50 mpaka lisaa 1; au mpaka mkate uive vizuri. Ukiiva, acha upoe kwenye chombo cha kuokea kwa dakika chache kisha hamishia kwenye waya wa kupozea keki upoe kabisa

Comments

Join discussion.