Muffin za ndizi ni nzuri sana haswa kwa watoto wanaenda shule kuwawekea kwenye snack boxes zao. Kufanya ziwe nzuri zaidi, punguza sukari na pia badala ya chocolate chunks, weka matunda makavu, berries au ndizi mbivu.

Yaliyomo kwenye ukurasa huu:

Dakika 30 Idadi ya walaji 6 Rahisi

Mambo ya kuzingatia

Siagi siyo lazima kwa muffins hizi. Endapo hauna siagi, tumia mafuta ya kupikia kipimo sawa na siagi. Mafuta katika uokaji wa muffins ni mazuri sana kwa radha nzuri na kiafya

Sukari inaweza kupunguzwa kwa wanaooka kwa ajili ya watoto au wasiopenda sukari. Kumbuka ndizi ni tamu sana tayari, ukipunguza sukari bado utapata utamu wa kutosha

Kuchanganya sana kunaharibu na kufanya muffins zisilainike vizuri. Ukiweka mchanganyiko wa unga wa ngano na viungo vikavu, changanya tu kuhakikisha hakuna weupe weupe na viungo vimechanganyikana vizuri, usizidishe zaidi ya hapo

Chocolate chunks siyo lazima kutumia. Badala yake tumia matunda yoyote kama berries, zabibu kavu, vipande vya ndizi na kadhalika. Hii itafanya ziwe nzuri zaidi kiafya

Kwenye kuoka, ili kupata muffins nzuri hakikisha umewasha oven na imepata joto kabla ya kuoka. Pia hakikisha oven imewasha kwenye setting ya joto la juu na chini

Hifadhi kwenye air tight container kwa siku moja nje ya friji au ndani ya friji kwa siku 5 mpaka 6. Unaweza pia kuzigandisha kwenye freezer mpaka miezi 3

Video

Angalia Video hapa jinsi ya kutengeneza hatua kwa hatua. Usisahau kusubscribe kwenye channel yetu ya YouTube

Mahitaji

Ndizi mbivu 3 wastani
1/2 kikombe sukari
1/4 kikombe siagi iliyoyeyushwa au 1/4 mafuta ya kula
1/2 kikombe maziwa ya mtindi/ mgando
Mayai 2 makubwa
Vijiko 1-1/2 vya chai vanilla
Vijiko 2-1/4 vya chai baking powder
1/2 kijiko cha chai mdalasini wa unga
1/4 kijiko cha chai chumvi
Vikombe 1-1/2 unga wa ngano
Kikombe 1 chocolate chunks/ chips (siyo lazima)

Maelekezo hatua kwa hatua

Hatua ya 1

Anza kwa kuwasha oven joto la 175 degrees C ili ipate joto wakati unachanganya unga. Paka mafuta chombo ca kuokea muffins au panga karatasi za kuokea endapo utatumia karatasi, weka pembeni. Ponda ndizi kwa kutumia uma, mwiko au kifaa chochote rahisi kwako mpaka zilainike vizuri; usitumie mashine tumia mkono, weka pembeni

Hatua ya 2

Ongeza sukari, siagi iliyoyeyushwa (ukikosa siagi tumia 1/4 kikombe mafuta ya kupikia), maziwa ya mgando/ mtindi na vanilla. Koroga mpaka ihcnganyikane kisha ongeza chumvi, mdalasini na baking powder. Changanya mpaka upate mchanganyiko mlaini

Hatua ya 3

Ongeza unga wa ngano, changanya mpaka tu uchanganyike vizuri. Haifai uchanganye sana, ukichanganya sana muffins zitakuwa ngumu. Tumia tu mwiko au kijiko cha kuchanganyia kuchanganya kwa dakika chache. Ukichanganyika ongeza chocolate chunks au chocolate chips kama utatumia

Hatua ya 4

Gawanya mchanganyiko kwenye vikopo 12 vya kuokea muffins vilivyojazwa ujazo wa theluthi 2…visijae sana wala visiwe na unga kiasi sana

Hatua ya 5

Oka kwa dakika 18 mpaka 22, au mpaka ukichomeka kijiti kitoka kisafi

Hatua ya 6

Ipua, acha zipoe kwa dakika 5 kwenye chombo cha kuokea kabla ya kuhamishia kwenye waya wa kupozea zipoe kabisa

Hatua ya 7

Enjoy

Comments

Join discussion.