Maini ya kuku ni mboga rahisi sana na tamu kama utaipatia kupika, na pia unaweza kuyachukia endapo utakosea kuipika. Jaribu recipe yatu utupe mrejesho
Yaliyomo kwenye ukurasa huu:
Dakika 30 | Idadi ya walaji 8 | Rahisi |
Mambo ya kuzingatia
Maini ya kuku ni tofauti na ya ngómbe. Maini ya kuku ni malaini zaidi, hivyo huiva kwa haraka zaidi na pia ni rahisi kumong´onyoka endapo utakosea kuyapika
Mafuta ni muhimu kwenye maini kama utataka yapendeze. Tumia mafuta mazuri kiafya kama Olive oil. Maini wakinyimwa mafuta hawapendezi
Kitunguu, pilipili hoho na karoti zinapendeza zikikatwa ukubwa unaokaribiana na ukubwa wa maini. katakata vipande vikubwa vikubwa vitakavyokaribiana na ukubwa wa vipande vya maini
Kaanga maini na mafuta, kitunguu saumu na tangawizi kwanza mpaka yaive ndio uchanganye kwenye sosi ya nyanya ili yasipondeke
Ongeza viungo utakavyopenda kama pilipili, ndimu, limao na vinginevyo kuongeza radha
Mbogamboga yani kitunguu, karoti na pilipili hoho zinapendeza zisipoiva sana na kubadilika rangi
Video
Angalia Video hapa jinsi ya kutengeneza hatua kwa hatua. Usisahau kusubscribe kwenye channel yetu ya YouTube
Mahitaji
Kilo moja maini
Vijiko 4 vya chakula mafuta ya kupikia
Kijiko 1-1/2 cha chakula kitunguu saumu na tangawizi
Chumvi kwa kuonja
Kijiko 1 cha chai binzari ya manjano
Kitunguu 1 kikubwa
Nyanya 3-4 za wastani
Karoti 1 kubwa
Pilipili hoho 1/2 x 3 rangi tofauti
Maji kiasi
1/2 kikombe majani ya kotimiri au giligilani
Maelekezo hatua kwa hatua
Hatua ya 1
Andaa viungo; katakata kitunguu, nyanya, pilipili hoho na karoti vipande vinavyokaribiana ukubwa wa maini. Visiwe vidogo sana wala vikubwa sana. Katakata na majani ya giligilani, weka pembeni
Hatua ya 2
Weka vijiko 3 vya chakula vya mafuta kwenye kikaango, yakichemka ongeza maini, kitunguu saumu na tangawizi pamoja na chumvi. Changanya vizuri, kuwa muangalifu unapochanganya na kugeuza maini yasimon´gonyoke. Geuza moja moja kwanza mpaka yote yapate rangi ya kahawia na yawe magumu kiasi ndio uyachanganye kwa pamoja. Kaanga maini kila upande kwa dakika 2 mpaka 3; au mpaka yawe na rangi nzuri ya kahawia na yaive ila yasiive sana yakakauka
Hatua ya 3
Pakua maini kwenye sahani, weka pembeni kisha ongeza kijiko 1 cha mafuta yaliyobakia kwenye kikaango
Hatua ya 4
Mafuta yakichemka ongeza kitunguu,kaanga mpaka kilainike ila kisikauke sana. Ongeza nyanya, karoti na chumvi kiasi ya kutosha kwenye nyanya. Funika na mfuniko, pika mpaka nyanya zilanike vizuri. Nyanya zikiiva unaweza kutoa maganda ya nyanya kama huyapendi
Hatua ya 5
Ongeza pilipili hoho na maji kiasi kama sosi itakuwa kavu sana. Kaanga kwa dakika kama 2-3 au mpaka pilipipi hoho ziive kiasi tu. Kama unapenda mchuzi mwingi, ongeza maji kiasi utakachopenda, acha yatokote kabisa ndio uweke maini
Hatua ya 6
Rudisha maini kwenye kikaanga uyachanganye vizuri na viungo vingine, mpaka yapate tu moto. Usiyaache yakae muda mrefu kwenye moto
Hatua ya 7
Ongeza majani ya giligilani, changanya vizuri. Ipua na kupakua
Hatua ya 8
Enjoy na chakula utakachotaka



Comments
Join discussion.