Hakuna kitu kizuri kama kujifurahisha wewe na uwapendao kwa kutengeneza na kupamba cookies nyumbani, haswa katika siku maalum kama birthdays, chirstmas, easter, Eid, mwaka mpya, anniversaries na kadhalikaDSC08790

Yaliyomo kwenye ukurasa huu:

Kuandaa dakika 5 Idadi ya cookies 20-26 Rahisi

Mambo ya kuzingatia

Vipimo Jaribu kufuatilia vipimo kama vilivyo. Tumia vikombe na vijiko maalum kwa kupimia ili kupata matokea mazuri zaidi

Maringue powder ndiyo inahitajika kwenye hii recipe siyo powdered egg whites.

Changanya kwa mashine ili kupata matokea mazuri zaidi. Maringue powder inafaa isagwe kwa speed kubwa kwa hiyo mashine ni muhimu sana

Maji ya limao siyo lazima. Kama hupendi limao tumia maji ya kawaida bila maji ya limao. Kwa hiyo vijiko 2 vya limao viwe maji badala yake

Tumia mifuko ya kupambia inasaidia sana kupata matokeo mazuri. Utahitaji pia vijiti vya meno (toothpicks)

Rangi za gel zinafaa zaidi kuliko rangi za maji au za unga kwa matumizi ya hii recipe

Video

Angalia Video hapa jinsi ya kutengeneza hatua kwa hatua. Usisahau kusubscribe kwenye channel yetu ya YouTube

Mahitaji

Vikombe 4 icing sugar
Vijiko 3 vya chakula maringue powder
Vijiko 7 vya chakula maji (na ya ziada yakihitajika)
Vijiko 2 vya chakula maji ya limao (na ya ziada yakihitajika)
Rangi tofauti za gel
Vipipi tofauti vya kupambia

Maelekezo hatua kwa hatua

Hatua ya 1

Weka icing sugar, maringue powder, maji na maji ya limao kwenye bakuli kubwa. Changanya na mashine mpaka ilainike na ibadilike iwe nyeupe sana na nzito

Hatua ya 2

Ongeza maji au maji ya limao taratibu mpaka upate uzito mzuri wa kupambia cookies. Endapo utazidisha maji ikawa nyepesi sana, ongeza icing sugar mpaka upate uzito sahihi

Hatua ya 3

Gawanya uweke rangi tofauti, kisha tumia kama itakavyohitajika

Comments

Join discussion.