Salad ni chakula kizuri sana chenye virutubisho vya kutosha. Salad inafaa kuliwa na watu wa kila rika na ni rahisi sana kutengeneza. Utamu wa salad unatokana mara nyingi na aina ya dressing utakayotumia. Mbali na dressing, muonekano wa salad na mvuto wake pia huchangia kwa kiasi kikubwa kuleta hamu ya kula. Leo tunatengeneza salad ya minofu ya kuku na dressing rahisi ya asali na apple cider vinegar!
DSC00160

Yaliyomo kwenye ukurasa huu:

Dakika 30 Idadi ya walaji 2 Rahisi

Mambo ya kuzingatia

Majani ya salad yapo ya aina nyingi tofauti. Unaweza kutumia unayopenda wewe na yanayopatikana kwa urahisi mahali ulipo. Unaweza pia kuchanganya majani ya aina tofauti kupata radha ya kiutofauti

Parachichi linafaa liwe limeiva vizuri na halijarojeka, liwe na vipande vizima vizima vitakavyoongeza mvuto kwenye sahani na radha wakati wa kula
DSC00174-copy

Kitunguu maji Kinaweza kukatwa kwa aina nyingi tofauti. Mimi napenda ya mduara, lakini unaweza kukata kama utakavyopendezwa. Kitunguu maji pia kinapendeza zaidi kikioshwa na kuondolewa ukali. Unaweza kuosha kawaida kwa kusugua na chumvi au osha na siki (vinegar) kama nilivyofanya kwenye video

Nyanya ndogondogo Zinapendeza sana kuliwa kwenye salad, na pia zinaongeza mvuta na hamasa ya kula. Unaweza kutumia nyanya za kawaida pia, chagua ambazo bado ngumu hazijaiva sana na kulainika
DSC00182-1

Mayai ya kuchemsha yanaongeza protein na utamu kwenye salad. Unaweza kuchemsha kutokana na upendeleo wako; yakaiva kabisa au yakabaki na ubichi kiasi

Mahindi yanaweza kutumika ya kopo au fresh kutokana na msimu. Mahindi na matamu na yana radha nzuri, ukikosa siyo lazima kutumia

Nyama ya kuku inaweza kuwa ya kukaanga, kuchoma au kuoka. Unaweza kuoka kwa kufuata recipe ya JikonaJane hapa au kukaanga kwa recipe hii

Viungo vya ziada kama matunda, nafaka, karanga, olives na kadhalika vinaweza kuongezwa kuboresha muonekano, radha na virutubisho
DSC00174-copy-2-1

Usafi ni muhimu sana kwenye utengenezaji wa vyakula vya matunda kwani ni rahisi sana kupata magonjwa kwenye utengenezaji wa salad na matunda. Tumia cutting board kwenye ukataji kuepuka kushikashika matunda, pia osha na kukausha matunda vizuri kabla ya kukatakata

Video

Angalia Video hapa jinsi ya kutengeneza hatua kwa hatua. Usisahau kusubscribe kwenye channel yetu ya YouTube

Mahitaji ya dressing

Kijiko 1 cha chakula Asali
Vijiko 2 vya chakula apple cider vinegar
Vijiko 3 vya chakula olive oil
3/4 kijiko cha chakula maji
1/4-1/2 kijiko cha chai chumvi
Pilipili manga kama itakavyohitajika

Mahitaji ya kiunguu maji

Kitunguu maji 1 cha wastani
Maji ya uvuguvugu kiasi
1/2 kijiko cha chai chumvi
Vijiko 1 cha vinegar nyeupe

Mahitaji ya salad

Majani ya salad kiasi chako
Parachichi 1
Nyanya ndogondogo kiasi chako
Yai moja la kuchemsha kwa kila sahani
Mahindi ya kopo kiasi
Chumvi na pilipili manga ikihitajika
Minofu ya kuku ya kukaanga kiasi. Recipe hapa

Maelekezo hatua kwa hatua

Hatua ya 1

Anza kwa kuchemsha mayai na kukaanga kuku kwa sababu anafaa kuku na mayai yawe yamepoa wakati unaweka kwenye salad ili joto lake lisiharibu majani ya salad. Kuku anafaa awe ameshawekewa viungo vyote, wakati unaandaa ni kumkaanga tu kwenye mafuta. Recipe ya kuku ipo hapa

Hatua ya 2

Wakati kuku anaendelea kupoa, andaa kitunguu maji. Unaweza kuosha kwa kutumia chumvi au loweka kwenye maji ya vinegar na chumvi kwa dakika 5 mpaka 10. Angalia video kwa maelekezo zaidi

Hatua ya 3

Andaa dressing. Koroga/ changanya viungo vyote vya dressing kwenye chupa, bakuli, kikombe au glass mpaka vichanganyikane vizuri. Funika hifadhi kwenye jokofu hadi itakapohitajika

Hatua ya 4

Osha na kukausha viungo vya salad vilivyobakia yani majani ya saladi, parachichi na nyanya. Katakata nyanya vipande viwili viwili kwa sababu ni ndogo. Emdapo utatumia nyanya kubwa, katakata vipande utakavyoona vinakututia. Katakata na parachichi pia vipande virefu nyembamba. Kama unatumia salad ya majani makubwa, na yenyewe katakata vipande vya wastani kwa kutumia mikono, huitaji kisu kukatakata. Katakata mayai vipande vinne vinne na minofu ya kuku vipande vya kutosha kuingia mdomoni

Hatua ya 5

Pangilia salad kwenye sahani yako, ukianza na kusambaza majani ya salad kwa chini, na juu panga nyanya, parachichi, nyama ya kuku na yai. Kisha ongeza kitunguu maji na mahidi kwa juu kama utakavyopenda.

Hatua ya 6

Miminia dressing kwa juu ila usiweke nyingi sana ikaharibu radha. Nyunyizia chumvi na pilipili manga kama itahitajika kwa juu. Enjoy
DSC00187-1

Comments

Join discussion.