Njia mojawapo ya kufurahia msimu wa maembe mbali na kuyala kama matunda, ni kutengeneza mango lassi (smoothie ya embe na iliki). Mango lassi ni kinywaji kinachoweza kufurahiwa na watu wa rika tofauti na pia ni kizuri kiafya
Yaliyomo kwenye ukurasa huu:
Dakika 5 | Idadi ya walaji 2 | Rahisi |
Mambo ya kuzingatia
Maziwa ya mgando mazito (greek yogurt) yanapendeza sana maana yanafanya smoothie inakuwa nzito. Ukikosa mazito (greek yogurt) unaweza kuchuja maziwa ya mtindi ya kawaida nyumbani. Weka kitambaa cha jikoni juu ya chujio kubwa, kisha weka chujio juu ya bakuli kwa ajili ya maji yatakayochujwa. Weka maziwa ya mtindi juu ya kitambaa. Funika acha ikae kwa lisaa 1 au zaidi. Yakishachujika tumia kama yanavyohitajika
Maziwa Fresh katika smoothies yenye full cream yanaongeza radha zaidi. Hata hivyo watu wanaofanya diet wanaweza kutumia maziwa ya low fat na wakafurahia smoothie yao
Kugandisha embe inawezekana kwa wanaopenda iwe ya baridi sana. Embe la kawaida bila kugandisha pia linafaa
Sukari siyo lazima haswa kama unawapa watoto wadogo. Pia kwa wasiotumia sukari wanaweza kuweka asali au maple syrup endapo utamu wa embe hautoshelezi
Watoto wadogo walioanza kula chakula pia wanaweza kunywa hii smoothie. Kuepuka kupata kifua, usigandishe matunda yao ili smoothie isiwe ya baridi sana
Hifadhi kwenye friji mpaka iwe ya baridi baada ya kutengeneza. Endapo utatumia embe la bila kugandisha
Video
Angalia Video hapa jinsi ya kutengeneza hatua kwa hatua. Usisahau kusubscribe kwenye channel yetu ya YouTube
Mahitaji
Vikombe 3 maembe, yaliyogandishwa
½ kijiko cha chai iliki
Vikombe 1½ maziwa
Kikombe 1 mtindi mzito
Kijiko 1 cha chakula sukari (ukipenda)
Maelekezo hatua kwa hatua
Hatua ya 1
Osha na kukatakata embe. Ukipenda iwe ya baridi sana, gandisha embe kabla ya kutengeneza
Hatua ya 2
Weka viungo vyote kwenye blender, saga mpaka ilainike vizuri
Hatua ya 3
Pakua kama utakavyopenda



Comments
Join discussion.