Smoothie ni kinywaji kitamu sana kinachohitaji viungo vichache na pia nzuri sana kwa afya. Ingawa ni kinywaji, smoothie hushibisha kama chakula. Kwa wanaopunguza uzito wanaweza kutumia maziwa ya mtindi na fresh low fat kutokana na matakwa yao.

Yaliyomo kwenye ukurasa huu:

Dakika 5 Idadi ya walaji 2 Rahisi

Mambo ya kuzingatia

Maziwa ya mgando mazito (greek yogurt) yanapendeza sana maana yanafanya smoothie inakuwa nzito. Ukikosa mazito (greek yogurt) unaweza kuchuja maziwa ya mtindi ya kawaida nyumbani. Weka kitambaa cha jikoni juu ya chujio kubwa, kisha weka chujio juu ya bakuli kwa ajili ya maji yatakayochujwa. Weka maziwa ya mtindi juu ya kitambaa. Funika acha ikae kwa lisaa 1 au zaidi. Yakishachujika tumia kama yanavyohitajika

Maziwa Fresh katika smoothies yenye full cream yanaongeza radha zaidi. Hata hivyo watu wanaofanya diet wanaweza kutumia maziwa ya low fat na wakafurahia smoothie yao

Kugandisha strawberries kunasaidia smoothie isiwe nyepesi sana, iwe ya baridi na pia ilete raha kunywa

Ndizi mbivu zina sukari sana ambayo inaleta utamu wa kutosha, kwa hiyo huitaji sukari. Ukipenda smoothie iwe nzito zaidi unaweza ukagandisha na ndizi pia

Watoto wadogo walioanza kula chakula pia wanaweza kunywa hii smoothie. Kuepuka kupata kifua, usigandishe matunda yao ili smoothie isiwe ya baridi sana

Kunywa haraka baada ya kutengeneza. Inawa unaweza kuhifadhi kwenye friji, ikiyeyuka inakuwa nyepesi na haipendezi tena

Video

Angalia Video hapa jinsi ya kutengeneza hatua kwa hatua. Usisahau kusubscribe kwenye channel yetu ya YouTube

Mahitaji

Vikombe 2 strawberries, zilizogandishwa
½ kikombe mtindi mzito
½ kikombe maziwa
Ndizi 2 ndogo au 1 kubwa

Maelekezo hatua kwa hatua

Hatua ya 1

Safisha na gandisha stawberries mpaka zigande kabisa

Hatua ya 2

Saga viungo vyote mpaka ilainike vizuri

Hatua ya 3

Kunywa wakati bado ya baridi

Comments

Join discussion.