Tambi za nyama ya kusaga au Fusilli bolognese ni chakula pendwa ambacho asili yake ni nchini Italia. Chakula hiki hipikwa na tambi za kuchemsha zinachangwanywa kwenye rosti ya nyama ya kusaga yenye nyanya na viungo vingine tofauti. Chakula hiki kinaweza kuliwa kama mlo kamili wa mchana au usiku. DSC00780

Yaliyomo kwenye ukurasa huu:

Dakika 50 Idadi ya walaji 6-8 Rahisi

Mambo ya kuzingatia!

Nyama ya kusaga inayotumika zaidi kwenye bolognese ni ya ng´ombe. Unaweza kutumia nyama ya aina nyingine. Ukitumia nyama ya kusaga ya kuku kumbuka uivaji wake ni tofauti, kuku ni laini inaiva haraka zaidi

Olive oil ndiyo mafuta ninayotumia mimi kwa sababu ni mazuri kiafya. Unaweza kutumia mafuta mengine yoyote unayotumia kila siku badala ya Olive oil

Nyanya na vitunguu ni moja ya viungo muhimu sana katika mapishi ya tambi za nyama ya kusaga, unaweza pia kuongeza na kupunguza kutokana na matakwa yako

Nyanya ya kopo inasaidia kufanya rosti iwe nzito zaidi. Unaweza kuongeza au kupunguza kutokana na matakwa yako

Macaroni/ pasta/ tambi zipo za aina nyingi sana, siyo lazima ziwe za aina moja. Tumia zinazopatikana mahali ulipo, hakikisha tu unachemsha kutokana na maelekezo ya kwenye pakiti kwa sababu zinatofautiana katika muda wa kuiva DSC00817-2

Majani ya basil yanaongeza radha kwenye tambi lakini siyo muhimu sana. Usihofu kutotumia endapo hayapatikani mahala ulipo

Cheese inapendeza sana kunyunyizia juu ya tambi baada ya kutenga mezani

Video

Angalia Video hapa jinsi ya kutengeneza hatua kwa hatua. Usisahau kusubscribe kwenye channel yetu ya YouTube

Mahitaji

DSC00833-2
Vijiko 4 vya chakula Olive oil
Kilo 1 nyama ya kusaga
Vijiko 2 vya chakula paste ya kitunguu saumu na tangawizi
Vijiko 4 vya chakula beef flavor
Pilipili manga kwa kuonja
Vitunguu maji 3 vya kawaida
Nyanya 4 ndogo/ za wastani
Kikopo 1 cha nyanya ya kopo
Maji kama yatakavohitajika
Vikombe 3 tambi
Chumvi kama itakavyohitajika
Majani ya basil

Maelekezo hatua kwa hatua

Hatua ya 1

Anza kwa kuandaa viungo. Katakata vitunguu maji vipande vya kawaida vya mraba. Katakata na nyanya kama utakavyopenda. Mimi napenda kukata nyanya moja mara 2, maganda natoa nyanya zikiiva. Chambua na majani ya basili, weka pembeni

Hatua ya 2

Ukiwa tayari kupika, chemsha sufuria au kikaango kwenye moto wa juu kiasi. Ongeza mafuta, nyama, paste ya kitunguu saumu na tangawizi, beef flavor na pilipili manga. Kaanga mpaka rangi ya ubichi iishe kwenye nyama, na nyama ianze kuiva

Hatua ya 3

Ongeza kitunguu maji, endelea kukaanga mpaka nyama iive vizuri na majimaji yote yakaukie kabisa

Hatua ya 4

Ongeza vipande vya nyanya kwenye nyama, pamoja na nyanya ya kopo na maji kama vikombe 2 na nusu. Changanya vizuri, acha nyama iive moto wa wastani kwa muda wa kama nusu saa; au mpaka nyama iive vizuri kabisa na nyanya zilainike

Hatua ya 5

Nyama ikikaribia kuiva, chemsha tambi/ macaroni/ pasta na maji na chumvi kiasi kama itakavyohitajika. Hakikisha huwivishi sana tambi/ macaroni/ pasta, pika kutokana na maelekezo ya kwenye pakiti. Zikiiva, chuja maji, weka pembeni.

Kumbuka, endapo utachemsha tambi kabla nyama haijaiva, zisuuze na maji ya baridi ili zisiendelee kuiva na mvuke zikawa kama ugali

Hatua ya 6

Nyama ikiwa tayari, ondoa maganda ya nyanya endapo ulikata mvipande vikubwa vikubwa. Ongeza tambi kwenye rosti ya nyama kisha uchanganye vizuri kabisa. Endapo sosi itakuwa kavu sana, ongeza maji kiasi mpaka upate sosi utakayopendezwa nayo

Hatua ya 7

Ongeza majani ya basil mwishoni wakati unaipua sufuria/ kikaango jikoni. Changanya vizuri

Hatua ya 8

Pakua kama utakavyopenda na cheese na kinywaji baridi

Comments

Join discussion.