Parfaits ni chakula chenye mvuto, kitamu na pia kizuri sana kiafya kutokana na viungo vyenye virutubisho vitumikavyo katika utengenezaji wake. Mbali na uvutiaji na ubora wake, chakula hiki ni rahisi sana kutengeneza, yani kinakuwa tayari ndani ya dakika tano. Leo tunatengeneza parfraits za maziwa ya mgando, strawberries, ndizi na asali.oo1

Yaliyomo kwenye ukurasa huu:

Dakika 10 Idadi ya walaji 2 Rahisi

Mambo ya kuzingatia

Aina ya matunda inategemea na mtengenezaji, walaji pamoja na msimu. Tumia matunda yanayopatikana na unayoyapenda wewe

Matunda sahihi ni yale ambayo hayajaiva sana. Yawe yameiva tu vizuri lakini siyo ya kubondeka yakaharibu muonekano na radha ukiyapanga kwenye glass. Matunda mazima mazima yanapendeza zaidi kuliko yaliyorojeka

Usafi ni muhimu sana kwenye utengenezaji wa vyakula vya matunda kwani ni rahisi sana kupata magonjwa kwenye utengenezaji wa matunda. Tumia cutting board kwenye ukataji kuepuka kushikashika matunda, pia osha na kukausha matunda vizuri kabla ya kukatakata

Asali siyo nzuri kiafya kwa watoto wa chini wa mwaka mmoja. Zingatia afya ya watoto kama una watoto wadogoDSC00017

Video

Angalia Video hapa jinsi ya kutengeneza hatua kwa hatua. Usisahau kusubscribe kwenye channel yetu ya YouTube

Mahitaji

Kikombe 1-2 maziwa ya mgando
Strawberries 3 kubwa
Kikombe 1 granola au muesli
Vijiko 2 vya chakula asali
Ndizi 1 ndogo

Maelekezo hatua kwa hatua

Hatua ya 1

Osha, kausha na katakata strawberries na ndizi vipande vidogo vidogo

Hatua ya 2

Andaa glass nzuri, anza kwa kuweka maziwa ya mgando chini ya glass, ongeza asali kiasi kwa juu kisha weka matunda kiasi halafu weka granola/ muelsi kwa juu. Rudia tena kuanza na maziwa ya mgando mpaka granola muesli; kutokana na ukubwa na urefu wa glass. Unaweza kurudia mara 2 mpaka 3

Hatua ya 3

Enjoy
DSC00012

Comments

Join discussion.